Picha za Ronaldo zinazoonyesha ustadi wake dhidi ya Uhispania

Ronaldo alifunga mabao matatu dhidi ya Uhispania katika mechi ambayo imesifiwa kuwa bora zaidi kuwahi kushuhudiwa katika Kombe la Dunia katika muda mrefu.

Mechi hiyo ilimalizika kwa sare ya 3-3, mabao ya Uhispania yakifungwa na Diego Costa (mawili) na Nacho.

Hapa, kwa picha, ndivyo mechi hiyo ilivyokuwa kwa Ronaldo.

ronaldo fouled for penalty Haki miliki ya picha AFP/Getty

Muda mfupi baada ya mechi kuanza, aliingia eneo la hatari na kujishindia penalti...

ronaldo scores first goal Haki miliki ya picha Reuters

... ambayo aliichapa upande wa kulia wa lango na kumbwaga kipa David De Gea, na kufunga dakika ya nne.

Ronaldo Haki miliki ya picha Reuters

Mchezaji huyo wa miaka 33 alionekana kuchagua ni wakati gani angehusika zaidi kwenye mechi, na wakati gani wa kuhifadhi nguvu zake uwanjani.

ronaldo scores second goal Haki miliki ya picha AFP/Getty

Baadaye kipindi cha kwanza, dakika ya 44, alimkanganya kipa De Gea tena, kwa mpira ambao uliiponyoka mikono ya kipa huyo wa Uhispania kama samaki mtelezi.

ronaldo celebrates scoring his second Haki miliki ya picha Reuters
ronaldo celebrates second Haki miliki ya picha AFP/Getty

Alisherehekea kwa kuteleza uwanjani, na kisha kufuatwa na wachezaji wenzake waliompongeza.

Ramos helps Ronaldo up Haki miliki ya picha AFP/Getty

Mechi hiyo ilikuwa imesifiwa kama mechi kati ya miamba, ambao mara nyingi hucheza wakiwa timu moja Real Madrid.

Lakini hakukuwa na uhasama kati ya Ronaldo na Sergio Ramos, Ramos akionekana wakati mmoja kumsaidia kuinuka uwanjani.

ronaldo hits free kick Haki miliki ya picha AFP/Getty

Dakika ya 88, Ureno walipata frikiki.

Ronaldo aliupinda mpira juu ya ukuta wa wachezaji wa Uhispania na ukatumbukia kwenye kona ndani ya wavu...

ronaldo after third goal Haki miliki ya picha AFP/Getty

... ambapo alinguruma uwanjani baada ya kutimiza hilo...

ronaldo celebrates goal Haki miliki ya picha EPA

... na kisha, kusherehekea kwa mtindo wake wa kipekee, kuruka juu na kuirusha mikono yake.

ronaldo embraces de gea Haki miliki ya picha EPA

Baada ya kipenga cha mwisho kupulizwa, alimkumbatia kipa wa Uhispania De Gea, ambaye alikuwa amemfunga mara tatu.

Wachezaji wa zamani walisifu uchezaji wake.

Sergio Ramos afunguka kuhusu kuumia kwa Mo Salah

Nahodha wa zamani wa Italia Franco Baresi alikosa maneno ya kuelezea uchezaji huo.

"Twende, familia!" alisema Ronaldo, akipigwa picha pamoja na timu baada ya mechi hiyo.

Picha zote zina haki miliki.