Kombe la Dunia 2018: Matukio kumi yanayokumbukwa zaidi Kombe la Dunia

Rudi Voller and Fank Rijkaard clash, Zinedine Zidane headbutts Marco Materazzi, Giorgio Chiellini reacts to a bite from Luis Suarez, Brazil react to their 7-1 humiliation by Germany Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Suarex kumng'ata Giorgio Chiellini, Zinedine Zidane kumgonga kwa kichwa Materazzi...

Kumetokea visa vingi vya kushangaza katika michuano ya Kombe la Dunia ambavyo daima vitasalia kukumbukwa na mashabiki wa soka. Hapa, tunaorodhesha matukio kumi yanayokumbukwa zaidi.

10. 2002 - Roy Keane atimuka kambini

Baada ya kutofuzu kwa kombe la dunia nchini Ufaransa 1998, Ireland iliingia dimba lililofuata nchini Korea Kusini na Japan mwaka wa 2002 kwa kishindo.

Timu hiyo ilikuwa na matumaini makubwa kwa Nahodha wa zamani wa Manchester United Roy Keane. Lakini mambo yaligeuka kinyume baada ya nyota huyo kundoka kambini Saipan ghafla na kwa ghadhabu.

Ilianzaje?

Walipotua tu katika kambi ya mazoezi, Roy Keane hakufurahishwa na huduma za mazoezi zilizowasilishwa. Hasira za mbabe huyo ziliongezeka baada ya mipira na vifaa vingine kuchelewa kufika. Kutokana na hali hiyo, Keane aliamua kuelekea nyumbani kabla ya kubadili uamuzi wake baadaye.

Mambo yaliharibika zaidi baada ya Keane kujibizana na kocha wake, Mick McCarthy katika mkutano wa kikosi.

Walioshuhudia matukio hayo hawajachelea kufichua yaliyotendeka.

Mshambuliaji wa zamani, Niall Quinn alisema: "Ni ukosoaji na kejeli niuliyowahi. Mick McCarthy alishtumiwa kuania mienendo yake, mbinu zake, mchezo wa timu na mchango wake na hata zaidi."

Wasimamizi wa timu waliamua kumtimua wenyewe kwa ukosefu wa nidhamu. Keane alirejea Ireland bila kugusa mpira nao wenzake wakifuzu raundi ya pili ambapo walichujwa na Uhispania.

9. 2002 - Korea Kusini, Italia na mwamuzi, 'Goli la dhahabu' la Korea laondoa Italia

Baada ya kufahamu kuwa watacheza dhidi ya Korea Kusini, Italia na kocha wake, Giovanni Trapattoni walijawa na matumaini na kuhisi kuwa na wapinzani hafifu.

Kilichofuata ni mshtuko mkubwa kwenye historia ya soka nje na ndani ya uwanja!

Yaliyotokia:

Italia iliongoza mechi hiyo kupitia bao la Christian Vieri na kushikilia uongozi hadi iliposalia dakika mbili mechi kukamilika ambapo Mchezaji wa zamani wa Wolves, Reading na Fulham Seol Ki-hyeon, aliposawazisha.

Katika kipindi cha ziada, Ahn Jung-hwan alitia kimiani goli la dhahabu lililowaliza Italia. Bao hilo lilimfanya Ahn kutimuliwa na klabu ya Italia ya Serie A, Perugia.

Kocha wa Korea Kusini wakati huo, Guus Hiddink alishtumu uamuzi huo na kusema ni hisia za kitoto. "Spoti inamaanisha wachezaji wote wanacheza katika mataifa tofauti ".

Ingawa baadaye aliitwa tena na Rais timu hiyo Luciano Gaucci, Ahn alikataa ualishi huo na kusakakta soka yake ligi ya Japan.

Bao hilo lilitanguliwa na tukio la kushtajaabiza pale Refa kutoka Ecuador Byron Moreno kuinyima Italia penalty, kukataa goli lingine akidai ni uoteaji na kumlisha Francesco Totti kadi nyekundu.

8. 2010 - Wachezaji wa Ufaransa wagoma

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Nahodha Patrice Evra aliongoza ususiaji huo 2010.

Ilivyotokea:

Ingawa walifuzu kushiriki kombe hilo kupitia bao la mkono la Thierry Henry dhidi ya Ireland, Ufaransa waliingia dimba hilo kama wanafainali kwani walipoteza kombe la dunia lililotangulia dhidi ya Italia kwa mikwaju ya penalty.

Licha ya kutoifungia timu ya taifa bao kwa mechi saba n ahata kwneye mechi ya uffunguzi dhidi ya Uruguay, Mfungaji wa Chelsea Nicolas Anelka alipewa nafasi katika safu ya kwanza ya mechi ya pili ya Ufaransa dhidi ya Mexico.

Tukio lenyewe.

Baada ya fomu kuendeleza fomu yake duni, kocha Raymond Domenech alimtoa katika kipindi cha pili. Ufaransa ilipoteza mchuano kwa mabao 2-0.

Sarakasi za Anelka ziliendelea baada ya kumtusi kocha Domenech kwenye chumba cha mabadiliko na kukataa kuomba msamaha. Hilo lilimfanya aondolewa kutoka timu hiyo iliyokuwa Afrika Kusini.

Kilikuwa kionjo cha sarakasi tu!

Kikosi cha Ufaransa kilitoa taarifa baadaye "kutofautiana na uamuzi wa Domenech".

Wachezaji walisusia kufanya mazoezi, na kurejea basini badala ya kuelekea uwanja wa mazoezi.

Domenech alifunguka: "Uamuzi wa kumchuja ni sahihi. Naomba msamaha kwa watoto ambao timu ya Ufaransa ina umuhimu mkubwa kwao''. Anelka hana haki ya kutoa matamshi hayo."

Ufaransa ilisalia mkiani kwenye kundi lao baada ya kuzabwa magoli 2-1 na wenyeji Afrika kusini katika mechi ya mwisho.

7. 1998 - Ronaldo na Fainali 1998.

Ilivyotokea:

Kombe la 1998 lingekuwa la tano la timu ya Brazil iwapo wangeshinda dhidi ya wenyeji Ufaransa.

'Atacheza au la?'

Tukio lenyewe:

Akiwa na umri wa miaka 21, Ronaldo alikuwa mchezaji ghali Zaidi duniani na nyota wa klabu ya Inter Milan. Hilo liliifanya kubeba matumaini ya taifa zima la Brazil kwa fainali hiyo ugani Stade de France.

Macho yalianza kupepeswa pale jina la Ronaldo, aliyekuwa na mabao manne katika shindano hilo, kukosekana kutoka kikosi cha fainali. Hali hiyo ilikarabatiwa na jina lake kurejeshwa katika wachezaji wa kuanza mechi. Licha ya yote, Brazil ililemewa na kufungwa 3-0 baada ya Ronaldo kusitasita uwanjani.

Ronaldo alijetetea: "Nilivurugika baada ya chakula cha mchana. Sijui kilichotokea, sikujihisi vizuri dakika chache kabla ya mechi. Hakuna aliyefahamu. "

Madai mbalimbali yanaonyesha kuwa huenda shirikisho la Brazil na wadhamini wa klabu hiyo walimlazimu ashiriki mechi hiyo licha ya kuwa na jeraha. Au hata Ronaldo alikuwa na tatizo la kimatibabu.

6. 1994 - Maradona na Mihadarati

Kabla tu ya dimba la 1994 nchini Marekani, Diego Maradona, alipigwa marufuku kwa kupatikana na hatia ya kutumia madawa yasiyoruhusiwa. Pia, alipewa kifungo kilichoahirishwa baada ya kuwafyatulia waandishi risasi.

Maradona aliingia shindano hilo baada ya kuisaidia Argentina kufuzu hatua ya fainali ya 1990 na kuwaongoza kutwaa kombe la dunia 1986.

Hata hivyo, Bahati yake iligeuka kuwa kinyume cha matarajio.

Mambo yalionekana kumuendea vyema Maradona baada ya kuifungia Argentina shuti safi dhidi ya Ugiriki.

Ishara alizotoa akisherehekea goli hilo iliwafanya wengi kutilia shaka hali yake ya afya. Licha ya yote, Nahodha huyo alijumuishwa mechi iliyofuata dhidi ya Nigeria.

Maradona hakujua yaliyomsubiri.

Mchuano huo ulikuwa wake wa mwisho akiwa na sera za Argentina. Staa huyo alichujwa kambini kwa kulifeli ukaguzi wa mihadarati. Alilishwa marufuku ya kutocheza miezi 15. Hali hiyo ilikwamiza safari yake na timu ya Argentina aliyoiwakilisha mechi 91.

"Wamenistaafisha kutoka soka. Sidhani ninahitaji kulipiza kisasi. Roho yangu imevunjika." Maradona alifunguka.

5. 1982 - Schumacher amshambulia Battiston

Ushindi wa Ujerumani magharibi dhidi ya Ufaransa katika nusu fainali ulihusisha mabao sita, manne katika muda wa nyongeza na mikwaju ya Penalti.

Licha ya mechi hiyo kutajwa kuwa miongoni mwa mechi bora katika kombe la dunia, ubora huo ulifutwa na tukio kati ya beki wa Ufaransa Patrick Battiston na kipa wa Ujerumani Harald Schumacher.

Baada ya kupokea pasi kutoka Michel Platini, beki Patrick Battiston wa Ufaransa aligongwa na kipa Harald Schumacher.

Battiston alipoteza meno mawili, kuumia mgongo, kupata jeraha la mifupa ya mabavu na kuhitaji gesi ya Oxygen.

Battiston alinena baadaye: "Ninachojua ni kuwa Schumacher ni mtu ambaye alitaka kushinda kwa udi na uvumba na hivyo basi kufanya hivyo."

Cha kustajaabisha ni kuwa refa, mholanzi Charles Corver hakupeana mkwaju wa akiba na Ujerumani walielekea fainali walipoadhibiwa na Italia mjini Madrid.

4. 1990 - Rijkaard amtemea mate Voller

Uhasimu wa kudumnu kati ya Ujerumani Magharibu na Uholanzi waliokutana fainali ya kombe la 1974, liliobebwa na Ujerumani, ulifufuliwa pande hizo zilipokutana kwenye hatua za mchujo nchini Italia 1990.

Ingwa mshambuliaji wa Ujerumani Rudi Voller na beki wa Uholanzi Frank Rijkaard walikutana katika mechi za ligi ya Italia ya Serie A, Voller amekuwa mhasiriwa wa matukio mawili mabaya kuwahi kushuhudiwa katika historia ya dimba hilo.

Kilichotokea:

Mchezaji wa AC Milan Rijkaard alilishwa kadi kwa kumchezea visivyo Voller na pindi tu wawili hao walipokuwa wakirejea mchezoni, Mholanzi Rijkaard alimtemea kohozi Voller.

Alipojaribu kumfahamisha refa yaliyofanyika, Voller mwenyewe aliadhibiwa kwa kadi ya njano.

Mkwaruzano wao uliendelea dakika moja baadaye. Refa Juan Carlos Loustau kutoka Argentina aliyeonekana kuchoshwa na mchezo wa wili hao, alimpokeza kila mmoja kadi nyekundu.

Donda la Voller lilidungwa msumari kwani alipokuwa akisimama kwa kustajaabishwa na hali hiyo, alitemewa kohozi nyweleni na Rijkaard.

Rijkaard said: "Nakiri siku hiyo nilikosea. Hakukuwa na matusi. Ninamuheshimu sana Rudi Voller ila tu nlipolishwa kadi nyekundu, hisia zangu zilizidi. Voller amenisamehe kwani baadaye nilimuoba msamaha. Nina furaha alikubali. Sina hisia mabaya dhidi yake."

Ujerumani Magharibu ilishinda kipute hicho, ikaiondoa Uingereza katika hatua ya nusu fainali kabla ya kuliinua kombe hilo kwa mara ya tatu kwa kuichapa Argentina katika finali.

3. 2014 - Ujerumani yawadhalilisha wenyeji Brazil

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption David Luiz akitokwa na machozi baada ya Brazil kuaibishwa na Ujerumani

Brazil, waliingia mechi hiyo wakiwa na ndoto za kuliinua taji lao la sita mbele ya mshabiki wao na kuzidisha sifa zao za kuwa timu ya soka yenye ufanisi mkubwa.

Historia pia iliegemea Brazil kwani, Kabla ya mechi hiyo, hawajawahi kufungwa nyumbani kwa miaka 39.

Nyota Neymar, alionekana kuwa kipaji chenye uwezo wa kuisaidia Brazil kuduisha historia hiyo pamoja na kutimiza ndoto hizo.

Hata hivyo, Brazil, yaani Selecao walitapatapa katika nusu fainali hiyo dhidi ya Ujerumani na hata kuwa bila huduma za Neymar na Thiago Silva waliojeruhiwa.

Kwenye dakika 18 za kwanza za mechi, Taifa na wapenzi wa soka duniani kwa jumla walisalia wakiduwaa kwa mshangao!

Kwa ustadi na ushirikiano, Ujerumani tayari ilikuwa imepachika mabao matano.

Udhalilishaji huu ulitekelezwa miaka miwili tu kabla ya Brazil kuwa wenyeji wa mashindano ya Olimpiki.

Ujerumani iliendeleza udunishaji huu katika kipindi cha pili na kufikisha idadi ya mabao hadi 7-0. Oscar aliipa Brazil bao moja lakini halikutosha kufuta machozi - yaani, kuondoa aibu!

"Ni siku mbaya zaidi maishani mwangu" alisema Kocha wa Brazil Luiz Felipe Scolari ambaye mwaka wa 2002 aliipa Brazil kombe lao la tano.

2. 2014 - Suarez amng'ata Chiellini

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Suarez amepigwa marufuku mara tatu kwa kuwang'ata wachezaji

Mabingwa mara nne Italia walikuwa kwenye hatari ya kutofuzu kwa hatua za mchujo kwa mara ya pili mfululizo baada ya kumaliza nafasi ya mwisho kwenye kundi lao 2010.

Baada ya kuisiaidia Uruguay kwa kuzuia goli kutumia mkono wake dhidi ya Ghana, Luis Suarez na Uruguay walushtumiwa vikali.

Zikiwa zimesalia dakika kumi kwenye mchuano wa Uruguay dhidi ya Italia, staraika Luis Suarez na beki wa Italia Giorgio Chiellini walianza kuwania mpira kwenye eneo la hatari.

Sekunde chache baadaye, Chiellini alifichua alama za kung'atwa kwenye bega lake. Isitoshe, mbali na kukana kutekeleza kosa hilo, Suarez alilalamika kupigwa kutumia kisugudi.

Uchungu wa Italia ulizidi kwani, licha ya refa kutokuchukua hatua yoyote dhidi ya Suarez, pasi ya mshambulizi huyo iliunganishwa na Diego Godin na kuipa Uruguay goli lililoitema Italia nje ya kombe hilo.

"Mambo hufanyika uwanjani, na si vyema kuyafanya yawe makubwa." Alisema Suarez.

Dua ya Chiellini zilikubalika pale FIFA ilipomfungia Suarez miezi minne nje ya soka.

Marufuku hiyo ni adhabu kubwa kuwahi kutolewa.

Suarez anadiwa kuwa na mazoea ya kuwang'ata wenzake kwani amewahi kuhusika katika vitendo vya aina hiyo hapo awali.

Zaidi ya yote...

1. 2006 - Zidane amgonga kwa kichwa Materazzi

Ni kipindi ambacho Zinedine Zidane alitangaza kuwa angestaafu baada ya dimba la dunia 2006.

Nyota na nahodha huyo aliisaidia Ufaransa kufika hatua ya fainali baada ya kuwapiga jeki kuinua kombe la dunia 1998 kupitia mabao yake mawili.

Taji hilo la 2006 pia lilionekana kuelekea Ufaransa. Mkwaju wa Zidane dakika ya saba iliiweka Ufaransa mbele kabla beki Marco Materazzi kusawazisha mambo dakika 12 baadaye.

Mchuano ulionekana kuelekea mikwaju ya penalti kabla ya Zidane na Materazzi kujibizana. Matokeo yalikuwa ni Materazzi sakafuni.

Ingawa kamera hazikunasa tukio nzima, picha za baadaye zilionyesha wawili hao wakirudushiana maneno. Zidane alimkarabia Materazzi na kumlima kichwa.

Punde si punde Refa Horacio Elizondo alimpokeza Zidane kadi nyekundu baada ya kuwasiliana na msaidizi wake.

Safari ya soka ya Zidane iliishia hapo huku hisia tofauti zikitolewa kuhusu tendo lake.

"Haikuonekana kama Materazzi alifanya kosa lolote - Lakini Zidane kuendelea na kufanya kosa kama hilo katika mechi kama hii, na mbele ya mamilioni ya watazamaji linashangaza." Mchanganuzi wa BBC Alan Shearer alisema:

"Linaudhi kwa Zidane,mchezaji wa haiba yake kumaliza taaluma yake hivyo. Ni yeye tu anaweza kufafanua kilichokuwa akilini mwake wakati huo kabla ya kufanya tendo," ameongeza Shearer.