Mkuu wa zamani wa soka Ghana ajitetea dhidi ya tuhuma za rushwa

Kwesi Nyantakyi Haki miliki ya picha AFP
Image caption Kwesi Nyantakyi alikuwa ameahidi kukabiliana na rushwa

Mwandishi wa habari za uchunguzi Anas Aremeyaw Anas, kutoka nchini Ghana, amekataa aliyekuwa rais wa shirikisho la soka la Ghana Kwasi Nyantakyi kwamba mtu fulani alimfuata na kumdai rushwa ya dola za Kimarekani laki moja unusu kwa lengo la kuzuia uchapishwaji wa taarifa ya ripoti ya ubadhirifu wa fedha na rushwa.

Katika taarifa ya utetezi wake binafsi, bosi huyo wa zamani wa chama cha soka amedai kwamba mwanashria aliye karibu na Anas alimfuata na kudai kiwango hicho cha fedha ili kufanikisha zoezi la kuzuia uchunguzi wa waraka huo.

Kama hiyo haitoshi, bwana Nyantakyi, amedai kuwa mwandishi huyo wa habari za uchunguzi na timu yake wali dakua barua pepe zake.

Lakini pia ameongeza kudai pia kuwa kiasi cha fedha za marekani dola elfu sitini na tano ambazo alionekana akiziingiza kwenye mfuko katika mkanda uliorekodiwa kwa siri hazikuwa za ushawihi bali dola elfu arobaini ambazo zilikuwa ni kwa ajili ya kujikimu kwa gharama za malazi katika zoezi zima la jitihada za Morocco kutaka kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia ya 2026.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kwasi Nyantakyi bosi wa zamani wa soka la Ghana ambaye ameachia ngazi nafasi hiyo baada ya kukabiliwa na tuhuma za rushwa

Katika taarifa ya kukabiliana na Anas Aremeya Anas amekataa madai hayo akidai kwamba bosi huyo wa zamani amepokea dola elfu sitini na tano kama rushwa, na kuongeza kuwa barua pepe za bosi huyo hazikusitishwa kwa muda kumfikia na mtu yeyote wa upande wake.

Wafanyakazi wengi wa tasnia ya soka na viongozi walikamatika kwa siri kwenye mkanda wa video wakipokea zawadi za fedha inaarifiwa katika waraka wa uchunguzi na kuwaacha wa Ghana walio wengi katika mshangao kutokana na hali hiyo.

Kwesi Nyantakyi, baada ya madai hayo kuibuliwa amejiuzulu nafasi yake ya raisi wa soka la Ghana FA, mjumbe wa FIFA,Umoja wa Soka Afrika Magharibi na hata CAF.Lakini vita vya maneno baina ya bwana Nyatakyi na Anas Aremeyaw Anas vinaendelea na huenda vikasababisha mvutano mkubwa na mrefu sana kisheria.

Image caption Kwenye video, anaonekana akichukua bunda la noti na kuziweka kwenye mfuko

Mada zinazohusiana