Caster Semenya kuwa mtetezi wa jinsia

Testeron issue Haki miliki ya picha Michael Dodge
Image caption Caster Semenya kwenda mahakamani kudai haki ya wanawake wenye viwango vya juu vya homoni

Mshindi wa dunia wa michuano ya Olimpiki wa mbio za mita mia nane Caster Semenya anatarajia kwenda mahakamani kwa lengo la kudai "haki" dhidi ya sheria zinazoathiri wanariadha wa kike wenye kiwango cha juu zha homoni za kiume .

Shirikisho la riadha ulimwenguni IAAF limeelekeza kuwa wanariadha wa kike wenye viwango vya juu vya homoni za kiume wanapaswa kuchuana na wanaume michezoni badala ya wanawake, ama wabadili michezo, vinginevyo wawe katika matibabu maalumu.

Semenya atafungua kesi katika Mahakama ya Usuluhisho wa Michezo, pia amenukuliwa akilalamika kuwa si haki, ninataka kuendelea kwenye riadha kama ilivyo kawaida yangu, vile nilivyozaliwa , ametoa ya moyoni mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka ishirini na saba kutoka nchini Afrika Kusini.

Anasema yeye ni Mokgadi Caster Semenya, anakiri kuwa yeye ni mwanamke tena mwenye kasi zaidi michezoni.

Mjadala wa viwango vya juu wa homoni .

Uamuzi huo, ambao unatarajiwa kuanza kutumika tarehe mosi Novemba mwaka huu, unawahusu wanariadha wanawake wanaokimbia kuanzia mita mia nne hadi maili moja.

Semenya, mshindi mara mbili wa michuano ya Olimpiki na mshindi mara tatu wa dunia katika riadha, siku za hivi karibuni amejikuta katika wakati mgumu pale alipopewa ushauri wa kwenye kufanyiwa uchunguzi na kiongozi mkuu wa riadha ulimwenguni kisha ajulikane yeye ni wa jinsi gani, ingawa mpaka sasa haijatanabahishwa hadharani dhidi ya jinsi yake.

Viwango vya juu vya homoni husababisha umbo la mwanamke kushupaa na kuonesha misuli,kuwa na nguvu nyingi, na kiwango cha juu cha chembe chembe nyekundu za damu kinyume na ilivyo zoeleka na huathiri kikomo cha uvumilivu.

Mwanasheria Norton Rose Fulbright atamuongoza Semenya katika suala zima la sheria , na inatarajiwa kufunguliwa huko Lausanne mwanzoni mwa wiki ijayo.

Imearifiwa kuwa Semenya kama walivyo wanariadha wengine, anapaswa kuchuana upande wa riadha kama alivyo zaliwa bila kumbagua ama kulazimishwa kubadilisha mwili wake kwa njia yoyote ya matibabu. "