Unamfahamu vipi kocha wa Senegal Aliou Cisse

Aliou Cisse

Chanzo cha picha, Khaled Desouki

Maelezo ya picha,

Aliou Cisse

Aliou Cisse alikuwa nahodha wa Senegal wakati walifuzu kwanza kabisa kwa kombe lao dunia mwaka 2002 na sasa ndiye kocha wao.

Jina lake ni maarufu miongoni mwa mashabiki wengi wa soka nchini Uingereza na pia miongoni mwa wale walio nchini mwake.

Cisse 42, alianzia taaluma yake ya kucheza kandanda na Lille OSC kabla ya kuhamia CS Sedan na kisha Paris Saint-Germain.

Alipanda ngazi kutoka kuwa naibu meneja hadi kaimu meneja na sasa amechukua usukani kamili wa timu.

Aliou Cisse alichezea klabu gani katika Ligi ya Primia?

Wakati Cisse alitoka Montpellier mwaka 2002 alijiunga na Birmingham kwenye Ligi ya Primia. Alipiga hatua kujijengea jina kama anayecheza mchezo "mchafu."

Cissea aliwekwa kwenye kikosi cha Arsenal wakati wa mechi ya kwanza lakini akafukuzwa uwanjani.

Licha ya kufukuzwa kwake kufutwa, alipewa kadi tano za njano kwenye mechi sita, na jumla ya kadi 10 za njano kabla ya mwaka mpya.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Aliou Cisse

Alionyesha mchezo mzuri msimu wote lakini akarejea amechelewa mazoezi ya msimu mpya mwezi Julai mwaka 2003 na kusababisha meneja kumuorodhesha kuwa wa kuuzwa.

Wakati wa mwisho wa msimu alijiunga na Portsmouth kwa pauni 300,000 kwa mkataba wa miaka miwili na kushinda ushindani mkali kutoka kwa mahasimu Bolton Wanderers.

Alimaliza taaluma yake nchini Ufaransa kwa kuzichezea Ardennes na Nimes.

Aliou Cisse amechezea nchi gani na amemuongoza nani?

Cisse alikuwa nahodha ya kikosi cha Senegal kilichofika robo fainali ya kombe la dunia la mwaka 2002 ambapo waliwashindwa wabingwa wa wakati huo Ufaransa.

Alikuwa pia sehemu ya kikosi cha Senegal kilichochukua nafasi ya pili katika kombe la taifa bingwa barani Afrika mwaka 2002 lakini alikuwa mmoja wa wachezaji waliopoteza penalti wakati wa fainali na kupoteza dhidi ya Cameroon.

Cisse aliteuliwa naibu kocha wa Senegal mwaka 2010 na kaiku meneja miaka miwili baadaye.