Morocco, Misri na Saudia zaondolewa katika Kombe la Dunia

Nahodha wa timu ya Morocco baada ya kushindwa na Portugal

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Nahodha wa timu ya Morocco baada ya kushindwa na Portugal

Boa la Luis Suarez kunako dakika ya 23 lilitosha kuisafirisha Saudi Arabia hadi nyumbani.

Uruguay ilipata ushindi wa 1-0 dhidi ya Saudi Arabia.

Wakati huohuo goli la Cristiano Ronaldo limeibeba Ureno na kuilazimu Morocco kuanza safari ya kuondoka Urusi.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Suarez baada ya kufunga bao dhidi ya

Ingawa bara Afrika lilijivunia ushindi wa Senegal siku ya Jumanne, matokeo ya Morocco yamebadili hisia baada ya Afrika kumpoteza mwakilishi mmoja. Afrika sasa ina timu nne.

Ingawa wamesalia na mechi moja, Morocco haina nafasi ya kufuzu kwa hatua ya muondoano.

Morocco, maarufu simba wa Atlas, waliingia mechi hiyo wakisaka ushindi wao wa kwanza baada ya kupoteza mechi yao ya ufunguzi dhidi ya Iran1-0.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mo Salah baada ya Misri kupoteza kwa Urusi siku ya Jumanne

Misri imebanduliwa katika michuano hiyo baada ya Uruguay kuilaza Saudia, na hivyobasi kukata tiketi ya raundi ya pili pamoja na waandalizi wa michuano hiyo Urusi.

Siku ya Jumanne Urusi iliicharaza Misri 3-1.

Wakati huohuo Kocha wa Morocco Herve Renard alifanya mabadiliko matatu, lakini hayakutosha kuisaidia Morocco dhidi ya Ureno.

Chanzo cha picha, Reuters

Kwa mara nyingine tena, bao la Ronaldo limeipa Ureno alama tatu muhimu zilizoipaisha hadi nafasi ya kwanza Kundi B.

Kufikia sasa, Ureno ina pointi nne kwa jumla.

Kwa nini Morocco imechujwa mapema?

Iran itakuwa na alama 6 iwapo itashinda dhidi ya Uhispania.

Uhispania kwa upande wake itakuwa na alama 4 iwapo itaifunga Iran.

Pande hizi zikitoka sare, Iran itakuwa na alama nne, nayo Uhispania ikiwa na alama 2.

Chanzo cha picha, Getty Images

Baada ya kucheza mechi mbili, Morocco haijapata alama au hata goli.

Timu hiyo itacheza mechi yake ya mwisho dhidi ya Uhispania.

Siku ya Ronaldo

Cristiano Ronaldo amegonga vichwa vya habari kwa mara nyingine baada ya kufunga goli lake la 85 akiichezea timu ya taifa.

Aidha, Ronaldo ndiye mchezaji anayeongoza orodha ya wafungaji bora wa magoli dimba la dunia

Timu ya Morocco imeonyesha mchezo mzuri mechini lakini haikuweza kufunga mabao.

Beki Benatia alipata fursa nyingi za kufunga ila hakuzitumia.

Kipa wa Ureno Rui Patricio, ameisaidia Ureno kwa kuzuia mikwaju ya Morocco.

Morocco imekuwa na mvuto mkubwa kutokana na juhudi zake uwanjani, huku wanasoka wake wakionyesha mchezo wa hali ya juu.