Hassanati Swaleh: Brazil iko kwenye damu yangu

Hassanati Swaleh: Brazil iko kwenye damu yangu

Bingwa mara tano wa kombe la dunia, Brazil, wana mashabiki wengi kote duniani, na katika kombe la dunia mwaka huu nchini Urusi mashabiki hao wanafuatilia kwa makini timu yao ambayo iko kundi E pamoja na Uswizi, Costa Rica na Serbia.

Mjini Mombasa pwani ya Kenya, Hassanati Swaleh ni miongoni mwa mashabiki sugu wa Brazil tangu utotoni mwake.

Hassanati ana matumaini mwaka huu Brazil italeta furaha kwenye nyuso zao baada ya kuambulia patupu kombe la dunia mwaka wa 2014 wakiwa nyumbani. Kichapo cha mabao 7-1 dhidi ya Ujerumani kilimpa presha Hassanati ambaye anasema hatasahau siku hiyo.

Alizungumza na mwandishi wa BBC John Nene mtaa wa Majengo, Mombasa.