Manchester United wamnunua nyota wa Brazil Fred anayechezea Shakhtar Donetsk kwa £47

Fred Haki miliki ya picha Getty Images

Manchester United imekamilisha usajili wa Kiungo wa Brazil Fred kwa kitita cha pauni 47.

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 25 ambaye anaiwakilisha Brazil nchini Urusi Kombe la Dunia, anajiunga na klabu hiyo kutoka Shakhtar Donetsk.

Amesaini mkataba wa miaka mitano.

Ni mchezaji wa pili kusajiliwa na Kocha Jose Mourinho kufuatia uhamisho wa Diogo Dalot kutoka FC Porto.

"Hii ni klabu bora duniani na ni furaha kubwa kujiunga nao," alisema Fred.

"Kufanya kazi na Jose Mourinho, ambaye ametwaa mataji mengi akiwa mkufunzi, ni fursa muhimu."

Mourinho amesema: "Fred ataongeza ujuzi kwenye kikosi chetu cha viungo wa kati, ujuzi unaohitajika; ubunifu wake na maono wakati wa kutoa pasi vitatupatia sura mpya kwenye uchezaji wetu."

Fred ameiwakilisha klabu ya ligi kuu ya Ukraine ya Shakhtar ambapo aliisaidia kubeba mataji ya ligi kuu mara tatu, kombe la Ukraine mara tatu na mataji manne ya Super Cup Ukraine.

Alijiunga nao kutoka klabu ya Internacional mnamo 2013 na kuwafungia mabao 15 kwenye mechi 155.

Msimu uliopita, Fred aliisaidia Shakhtar kufika hatua ya muondoano Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Fred alishiriki kwenye ushindi wa Shakhtar dhidi ya Manchester City na Napoli, na kufunga goli dhidi ushindi wa 2-1 dhidi ya Roma hatuaya 16 bora.

Kufikia sasa Fred hajashiriki Kombe la Dunia licha ya kuwa kwenye wachezaji wa akiba dhidi ya Uswizi.

Mechi hiyo ya ufunguzi ilikamilka sare ya 1-1.

Mada zinazohusiana