'Mimi kama mwanamke niliguswa na msichana aliyekuwa analia'
Huwezi kusikiliza tena

Mtanzania Alice Ahadi Magaka alivyopata wazo lililomshindia Tuzo ya Malkia

Tuzo ya Malkia wa Uingereza kwa viongozi vijana hutolewa kila mwaka kama njia moja ya kuitambua kazi inayofanywa na vijana katika jamii mbalimbali za mataifa ya Jumuiya ya Madola.

Vijana waliofanikiwa huletwa Uingereza ili kukutana na wafanyabiashara mbalimbali na pia kupata nafasi zaidi ya kubadilishana mawazo.

Kati ya walioalikwa mwaka huu ni Alice Ahadi Magaka, kutoka Tanzania, ambaye alitutembelea katika studio zetu hapa London. Anaanza kwa kuelezea mradi wake unahusu nini.