Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 23.06.2018

Nabil Fekir Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mchezaji wa kiungo cha kati wa Lyon Nabil Fekir,

Real Madrid wana hamu ya kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Lyon Nabil Fekir, huku Liverpool ikiwa katika hatari ya kumkosa mchezajihuyo mwenye umri wa miaka 24 mchezaji wa timu ya taifa ya Ufaransa. (RT France - Mirror)

Arsenal imefanya mazungumzo na mchezaji wa Sevilla na timu ya taifa ya Argentina Ever Banega, kuhusu uhamisho kuelekea Emirates. (Star)

Manchester City na Paris St-Germain wana hamu ya kumsajili mchezaji wa Bayern Munich mwenye umri wa miaka 29 kiungo cha ulinzi - Jerome Boateng. (Sport Bild - Manchester Evening News)

Chelsea wanaelekea kupunguza malipo kwa kumfuta meneja Antonio Conte kwa kutuhumu kwamba hakushughulikia vizur kuuzwa kwa Diego Costa. (Express)

Manchester City wanaelekea kukaribia ufanisi wa usajili wake wa kwanza wa msimu wa joto baada ya mzungumzo mazuri kuhusu mchezaji wa kiungo cha kati wa Napoli Jorginho, 26. (Manchester Evening News)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mchezaji wa kiungo cha kati wa Ujerumani Ilkay Gundogan

Manchester City inajitayarisha kuidhinisha mazungumzo kuhusu kandarasi mpya ya mchezaji wa kiungo cha kati wa Ujerumani Ilkay Gundogan, ambaye pia amehusishwana uhamisho kwenda Barcelona. (Sun)

Meneja wa Rangers Steven Gerrard ana hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Nigeria anayeichezea Roma Umar Sadiq, mwenye umri wa miaka 21. (Sky Sports)

Tottenham wamehusishwa na uhamisho wa mshambuliaji wa Ufaransa wa timu ya Nice Alassane Plea, mwenye umri wa miaka 25, huku meneja wa Spurs Mauricio Pochettino akionekana kumpa ushindani Harry Kane. (Foot Mercato - Sun)

Borussia Monchengladbach wameanzisha mazungumzo ya kumsajili Plea, anayeandamwa pia na Tottenham. (Nice-Matin - Talksport)

Liverpool wamedokezewa kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Stoke City na Switzerland Xherdan Shaqiri. (Express)

Matumaini ya Reading kumsajili Tommy Elphick wa Aston Villa yamegonga mwamba huku Villa ikitafakari mustakabali wa mchezaji huyo wa England. (Reading Chronicle)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wilshere aliikosa nafasi kuichezea timu ya England katika kombe la dunia

Mchezaji wa kiungo cha kati wa England Jack Wilshere, ataamua kuhusu mustakabali wake akiwa mapumzikoni baada ya kuondoka Arsenal. (Talksport)

Mesut Ozil wa Arsenal ataomba kuvaa kazi nambari 10 baada ya Wilshere kuondoka. (Mail)

Sevilla itamuwania mchezaji wa Newcastle United Mikel Merino, mwenye umri wa 22, iwapo Ever Banega, wa miaka 29, wa Argentina atakamilisha uhamisho wake kwenda Arsenal. (Northern Echo)

Fulham imewasilisha ombi la thamani ya £ milioni 10 kwa mchezaji wa Southampton beki kushoto Matt Targett. (Sky Sports)

Norwich wana hamu ya kumsajili mshambuliaji wa Sheffield Jordan Rhodes, wa miaka 28, baada ya kuuzwa kwa James Maddison, kwenda Leicester City. (Mirror)

Mkuu wa Crystal Palace Roy Hodgson, aliyemsimamia mchezaji wa kiungo cha kati wa Chelsea Ruben Loftus-Cheek kwam kopo msimu huu, anaamini mchezaji huyo wa miaka 22 ana uweledi zaidi kuliko aliyekuwa mchezajiw a timu ya taifa ya Ujerumani Michal Ballack. (Mail)

Pablo Zabaleta, wa Argentina anasema timu ya taifa hilo katika kombe la dunia inaonekana 'imevunjika moyo'. (Times)

Image caption Lionel Messi alitarajiwa kujitwika kapu la matumaini ya Argentina katika Kombe la Dunia

Meneja wa Ubelgiji Roberto Martinez anasema mshambuliaji Romelu Lukaku, wa miaka 25, hana lengo la kushinda tuzo la the Golden Boot katika Kombe la dunia, badala yake anataka kuisaidia timu hiyo. (Guardian)

Muuguzi mkuu wa timu ya taifa ya Urusi anasema anaweza kubashiri, 'chupa ya maziwa ya mgando', kuwa timu hiyo mwenyeji wa mashindano hayo walifanyiwa uchunguzi angalau mara mbili zaidi ya timu ya Uingereza kuonekana iwapo wanatumia madawa yoyote. (Telegraph)

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii