Salah apewa uraia wa heshima na kiongozi wa Chechnya

Mohamed Salah, raia wa heshima wa Chechnya
Image caption Mohamed Salah, raia wa heshima wa Chechnya

Kiongozi wa Chechnia, Ramzan Kadyrov ametangaza kumpatia uraia wa heshima wa Urusi mshambuliaji wa Liverpool na timu ya taifa ya Misri, Mohamed Salah

Salah yuko nchini Urusi kwene michuano ya kombe la dunia akiiwakilisha Misri, ambaye kambi yake ya mazoezi ipo mjini Grozny,Chechnya

Kadyrov amekuwa akikosolewa, akishutumiwa kumtumia mchezaji huyo kwa propaganda zake za kisiasa.

Utawala wa Kadyrov umekosolewa kwa kile kinachodaiwa kuwa ukiukaji wa haki za binaadamu, maai ambayo ameyakana juma hili alipozungumza na BBC.

"Mohamed Salah ni raia wa heshima wa Chechnya! ndio!'' Kadyrov aliandika siku ya Ijumaa.

''Katika hafla ya chakula cha jioni nilipatia heshima hiyo nikampatia Mohamed Salah nakala ya tangazo na beji.Amestahili''.

Salah alikosa goli wakati wa mchezo kati ya Misri na Uruguay wakati ambapo akiendelea kuuguza jeraha lake la bega.

Tifa hilo la Afrika litaikabili Saudi Arabia mjini Volgograd siku ya Jumatatu.