Tetesi za soka Ulaya Jumanne 26.06.2018

Paul POgba

Chanzo cha picha, Getty Images

Paris St-Germain imewapatia Manchester United ombi la mkataba wa kubadilishana kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba ,24, kwa beki wa Itali Marco Verratti pamoja na fedha.. (Sun)

Mshambuliaji wa West Ham Manuel Lanzini, 25, anatarajiwa kukosa msimu wote ujao kutokana na jeraha la goti alilopata wakati wa mazoezi nchini Argentina kabla ya mechi ya kombe la Dunia. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Manchester United inaweza kumpatia raia wa Uingereza Luke Shaw, 22, kandarasi mpya kwa sababu klabu hiyo haiko tayari kulipa dau la £60m kumsajili beki wa kushoto wa Juventus na Brazil Alex Sandro, 27. (Manchester Evening News)

West Brom imekataa ombi la £12m kutoka kwa West ham ili kumnunua beki wa Uingereza Craig Dawson, huku klabu hiyo ikisema kuwa mchezaji huyo ana thamani ya £20m. (Telegraph)

Chanzo cha picha, Getty Images

Sevilla imesisitiza kuwa kiungo wa kati Ever Banega, 29, hauzwi msimu huu licha ya hamu kutoka kwa Arsenal (Independent)

Lyon inajiandaa kumpatia Nabil Fekir, 24, mkataba mpya ili kuizuia Liverpool kufufua matumaini ya kumsaka mshambuliaji huyo wa Ufaransa. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Na rais wa Lyon Jean-Michel Aulas amesema kuwa amezungumza na mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho, ambaye huenda amejiandaa kuwasilisha ombi la kumnunua Fekir. (Bein Sports, via Manchester Evening News)

Babake Eden Hazard aliwasilisha ombi la kutaka mchezaji huyo kununuliwa na Real Madrid siku chache kabla ya fainali za kombe la klabu bingwa. (Marca)

Chanzo cha picha, Getty Images

Chelsea haijajiandaa kumuuza kiungo wa kati wa Uingereza Ruben Loftus-Cheek msimu huu lakini huenda ikakubali mchezaji huyo, 22, aliyeichezea Crystal Palace kuendelea kucheza kwa mkopo. (Mail)

Leicester City imewasilisha ombi la £12m ili kumnunua mchezaji wa Besikitas 29, Domagoj Vida, ambaye anaichezea Croatia katika kombe la dunia (Sabah, via Leicester Mercury)

Chanzo cha picha, Getty Images

Wolves inamtaka beki wa Lazio na Brazil mwenye umri wa miaka 23 Wallace, ambaye ni mteja wa ajenti Jorge Mendes. (Birmingham Mail)

West Ham itamtuma beki wa kulia wa Uingereza Sam Byram, 24, kwa mkopo wa muda mrefu kwa klabu ya Nottiingham (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images

Mabingwa wa ligi ya Itali Juventus wanakaribia kukamilisha kuandikisha mkataba na klabu ya CSKA Moscow na kiungo wa kati wa Urusi Aleksandr Golovin, 22, lakini hawana haja na kiungo wa kati wa Arsenal anayeondoka Jack Wilshere, 26. (Goal)

Chanzo cha picha, Getty Images

Beki wa Borussia Dortmund mwenye umri wa ,miaka 26 Erik Durm atafanyiwa ukaguzi wa kimatibabu na klabu ya Huddersfiedl wiki hii (Kicker - in German)

Chanzo cha picha, Getty Images

Southampton iko tayari kulipa £17.6m ili kumnunua mshambuliaji wa Barcelona Paco Alcacer, 24 lakini inakabiliwa na ushindani mkali wa kumnunua mchezaji huyo kutoka kwa klabu ya Uturuki Fenerbahce. (Mundo Deportivo - in Spanish)

Na Alcacer pia hataki kuondoka Barcelona licha ya klabu hiyo kutaka kumuuza na hivyobasi kuzuia uhamisho wowote muhimu.

Tetesi za Jumatatu 25.06.2018

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Hazard amesisitiza ameridhika Chelsea, ingawa amehusishwa na kuhamia Real Madrid

Kiungo wa kati wa Chelsea na Ubelgiji Eden Hazard, 27, alitaka kuuziwa Real Madrid kabla ya fainali ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kuchezwa mwezi Mei.

Babake ambaye pia ni mwakilishi wa mchezaji huyo Thierry Hazard anadaiwa kuwasiliana na Real Madrid kabla ya fainali hiyo mjini Kiev, Madrid akisema mazungumzo ya mkataba mpya kati ya Hazard na Chelsea yamekwama hasa ikizingatiwa hawachezi Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya msimu ujao (Marca)

West Ham wako tayari kumpa kiungo wa kati wa England Jack Wilshere mkataba wa mwaka mmoja pekee kwa sababu wana wasiwasi kuhusu uwezo wake wa kukaa bila majeraha. Wilshere mkataba wake katika klabu ya Arsenal unamalizika majira haya ya joto. (Sun)

Meneja mpya wa klabu ya Everton Marco Silva huenda akaamua kuwauza wachezaji nyota wa klabu hiyo ya Everton - wakiwemo kiungo wa Ufaransa Morgan Schneiderlin, 28, winga wa Congo Yannick Bolasie, 29, beki wa Wales Ashley Williams, 33, na mshambuliaji wa zamani wa England Wayne Rooney, 32. (Star)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Yannick Bolasie

Winga wa Newcastle na Scotland Matt Ritchie, 28, yuko tayari kurejea Bournemouth,huku mshambuliaji wa Norway Josh King, 26, naye akitarajiwa kwenda Newcastle. (Sun)

Uhamisho uliopendekezwa wa Riyad Mahrez kutoka Leicester kwenda Manchester City unachelewa kwa sababu kiungo wa kati huyo wa Algeria mwenye miaka 27 anataka alipwe kitita kikubwa cha pesa na Leicester ndipo akubali kuondoka. (Sun)

Mchezaji wa Ubeligji Marouane Fellaini, 30, amefichua kwamba utata kuhusu mkataba wake utatatuliwa hivi karibuni. Kiungo huyo wa kati wa Manchester United atakuwa bila mkataba hivi karibuni lakini amepokea ofa kutoka kwa klabu kadha. (Independent)

Kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba, 25, amekiri kwamba alikuwa na "matatizo madogo" na meneja wa Manchester United Jose Mourinho msimu uliomalizika hivi majuzi. (ESPN)

Kiungo wa kati wa Guinea Naby Keita, 23, anatarajiwa kurithi jezi nambari nane iliyokuwa ya Steven Gerrard katika klabu ya Liverpool.(Liverpool Echo)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Uhamisho wa Paul Pogba watiliwa shaka na Fifa

Meneja wa zamani wa Napoli Maurizio Sarri anapanga kuwa akiishi katika uwanja wa mazoezi wa klabu hiyo atakapojiunga na klabu hiyo baadaye wiki hii. (Mirror)

Mshambuliaji wa Manchester City Sergio Aguero, 30, huenda akatupwa nje ya kikosi cha kuanza mechi Argentina watakapojaribu kufufua matumaini ya kuendelea kucheza Kombe la Dunia dhidi ya Nigeria Jumanne. Kocha wa Argentina Jorge Sampaoli inatarajiwa huenda akajiuzulu au afutwe kazi baada ya michuano hiyo. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Sergio Aguero