Argentina yaitupa nje Nigeria kombe la dunia kwa ushindi wa 2-1

Messi na Rojo wakishangilia baada ya goli la ushindi
Image caption Messi na Rojo wakishangilia baada ya goli la ushindi

Mkwaju wa Marcos Rojo katika dakika za majeruhi ndiyo ulioziumiza roho za waafrika wengi na kupeleka furaha kwa wa Argentina wakivuka kwa shangwe kuelekea katika hatua ya 16 bora ya Kombe la Dunia la 2018.

Kama si mlinzi wa Manchester United Rojo kusogea katika eneo la hatari la Nigeria na kuipokea mpira uliopigwa na Gabriel Mercado, Argentina ilikuwa hoi kuelekea kuondolewa katika michuano hiyo mikubwa ya mpira wa miguu Duniani.

Lionel Messi ambaye alikuwa amefunga goli safi la kwanza, alimrukia Roho mgongoni kwa furaha, wakiungana na wenzao waliokuwa kwenye benchi la ufundi katika kushangilia ushindi.

Yalikuwa matokeo waliyostahili baada ya kuwa wamecheza vibaya katika kipindi cha pili kiasi cha kosa lililofanywa na Javier Mascherano kusababisha Nigeria kusawazisha kupitia mkwaju wa penati uliotiwa kimiani na Victor Moses anayechezea klabu ya Chelsea ya England.

Image caption Lionel Messi alizawadiwa kiatu cha dhahabu michuano ya kombe la dunia 2014

Nahodha wa Argentina Lionel Messi ambaye katika mechi hii alikuwa na jukumu la ziada kama kiongozi kutokana na mgogoro uliopo kati ya wachezaji na mwalimu Jorge Sampaol, amesema, "Ninawashukuru watu wote walioko hapa, kwa kujitolea kwao, na wale walioko nyumbani Argentina ambao muda wote walikuwa nasi"

Naye nahodha wa Nigeria John Obi Mikel amesema, " Tumefanya kila tuliloliweza.Katika kipindi cha pili tumepambana na kupambana. Basi tu haikuwa. Hii ni timu changa na katika miaka minne ijayo wengi wao watakuwa tayari kwa michuano hii".Ninajivunia vijana hawa na tulichokifikia. Nadhani tumefanya vizuri sana. Tunapaswa kusonga mbele"

Vigezo vitakavyotumika timu kufuzu awamu ya muondoano Kombe la dunia

Ni lini taifa la Afrika litashinda Kombe la Dunia?

Messi anakuwa mchezaji wa tatu wa Argentina kuwahi kufunga katika michuano mitatu ya Kombe la Dunia (2006, 2014 na 2018) baada ya Diego Maradona (1982, 1986 na 1994) na Gabriel Batistuta (1994, 1998 na 2002).

Image caption Mchuano huu ulikua na mvuto wa aina yake

Nusu ya idadi ya magoli yake 6 ya Kombe la Dunia, ameifunga Nigeria.

Bila shaka baada ya mchezo huu, mambo mawili yataendelea kuwa gumzo ni pamoja na afya ya afya ya Diego Maradona ambaye pamoja na vibweka kadhaa uwanjani, inadaiwa amekimbizwa hospitali mara ya mchezo.

Image caption Msimamo wa kundi D baada ya michezo ya mwisho

Jambo la pili la kimjadala itakuwa ni kuhusiana na iwapo Nigeria walistahili kupata Penalti wakati Rojo alipoupiga kwa kichwa mpira na mpira huo ukamgusa mgono kabla ya mwamuzi Cuneyt Cakir kwa msaada wa teknolojia ya video kuamua kuwa siyo penati.

Sasa Argentina watakutana na mshindi wa kundi C, Ufaransa, wakati mshindi wa kundi D Croatia ambaye ameishikilia nafasi ya kwanza baada ya kuwabamiza Iceland 2-1, akikwaana na Denmark.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii