Tetesi za soka Ulaya Jumatano 27.06.2018

Haki miliki ya picha Getty Images

Real Madrid inapanga kumuuza kiungo wa kati wa Uhispania Marco Asensio, 22, ili kutafuta fedha za kumnunua mshambuliaji wa PSG na Brazil Neymar, 26. Liverpool ina hamu ya kumsajili Asensio. (Sport - in Spanish)

Chelsea imewasilisha ombi la dau la £35m kumnunua beki wa Juventus Daniele Rugani, 23. Klabu hiyo inatumai kwamba raia huyo wa Itali atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na mkufunzi Maurizio Sarri. (Evening Standard)

Marouane Fellaini Haki miliki ya picha Getty Images

Kiungo wa kati wa Manchester United Marouane Fellaini atatoa tangazo kuhusu hatma yake mnamo tarehe mosi mwezi Julai. Raia huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 30 hajakubaliana na masharti ya klabu hiyo kuhusu mkataba mpya. (Manchester Evening News)

Jack Grealish, 22, yuko tayari kuondoka Aston Villa msimu huu ili kurudi katika ligi kuu ya Uingereza, huku Tottenham ikiongoza katika kutaka kumsajili mshambuliaji huyo wa Uingereza (Mirror)

Sokratis Papastathopoulos Haki miliki ya picha Getty Images

Arsenal inakaribia kumsaini beki wa Borussia Dortmund Sokratis Papastathopoulos, 30, huku ikiendelea na mazungumzo ya kutaka kumsajili beki wa Freiburg na Uturuki Caglar Soyuncu, 22. (Sky Sports)

Manchester United inamchunguza beki wa Itali na AC Milan Leonardo Bonucci, 31. (Yahoo)

Aaron Mooy, Haki miliki ya picha Getty Images

Manchester City inatazama uwezekano wa kumsaini kiungo wa kati wa Australia Aaron Mooy, 27, kutoka Huddersfield . City pia ina mpango wa dau la £20m huku Everton, West Ham United na Southampton pia wakipanga kumnunua Mooy. (ESPN)

Divock Origi Haki miliki ya picha Getty Images

Liverpool itamchunguza mshambuliaji wake wa Ubelgiji Divock Origi ,23, katika kipindi cha wiki chache zijazo na kumpatia fursa kuonyesha umahiiri wake katika klabu hiyo. Origi alihudumu msimu uliopita akicheza kwa mkopo katika klabu ya Wolfsburg Ujerumani. (Liverpool Echo)

Wolves wamekataa ombi la dau la £12m kwa mshambuliaji wa Fulham na raia wa Ureno Ivan Cavaleiro, 24, (Sky Sports)

Craig Dawson Haki miliki ya picha Getty Images

West Brom haimtaruhusu beki wa Uingereza Craig Dawson kuondoka katika klabu hiyo kwa gharama ya chini. Klabu hiyo ilikataa dau la £12m kutoka West Ham kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Sky Sports)

Stoke City wanakaribia kuweka mkataba na winga wa West Brom na Jamhuri ya Ireland James McClean, 29, baada ya kuimarisha dau la kwanza la £4m bid. (Mail)

Marcelo Bielsa Haki miliki ya picha Getty Images

Mkufunzi wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola yuko tayari kumsaidia Marcelo Bielsa katika klabu ya Leeds kumpatia baadhi ya wachezaji wake kwa mkopo . (Sun)

Sporting Lisbon itamfuta kazi mkufunzi wake Sinisa Mihajlovic, siku chache tu baada ya kuajiriwa.(Record)

Tetesi bora za Jumanne

Paul POgba Haki miliki ya picha Getty Images

Paris St-Germain imewapatia Manchester United ombi la mkataba wa kubadilishana kiungo wa kati wa Ufaransa Paul Pogba ,24, kwa beki wa Itali Marco Verratti pamoja na fedha.. (Sun)

Mshambuliaji wa West Ham Manuel Lanzini, 25, anatarajiwa kukosa msimu wote ujao kutokana na jeraha la goti alilopata wakati wa mazoezi nchini Argentina kabla ya mechi ya kombe la Dunia. (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images

Manchester United inaweza kumpatia raia wa Uingereza Luke Shaw, 22, kandarasi mpya kwa sababu klabu hiyo haiko tayari kulipa dau la £60m kumsajili beki wa kushoto wa Juventus na Brazil Alex Sandro, 27. (Manchester Evening News)

West Brom imekataa ombi la £12m kutoka kwa West ham ili kumnunua beki wa Uingereza Craig Dawson, huku klabu hiyo ikisema kuwa mchezaji huyo ana thamani ya £20m. (Telegraph)

Haki miliki ya picha Getty Images

Sevilla imesisitiza kuwa kiungo wa kati Ever Banega, 29, hauzwi msimu huu licha ya hamu kutoka kwa Arsenal (Independent)

Lyon inajiandaa kumpatia Nabil Fekir, 24, mkataba mpya ili kuizuia Liverpool kufufua matumaini ya kumsaka mshambuliaji huyo wa Ufaransa. (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images

Na rais wa Lyon Jean-Michel Aulas amesema kuwa amezungumza na mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho, ambaye huenda amejiandaa kuwasilisha ombi la kumnunua Fekir. (Bein Sports, via Manchester Evening News)

Babake Eden Hazard aliwasilisha ombi la kutaka mchezaji huyo kununuliwa na Real Madrid siku chache kabla ya fainali za kombe la klabu bingwa. (Marca)

Haki miliki ya picha Getty Images

Chelsea haijajiandaa kumuuza kiungo wa kati wa Uingereza Ruben Loftus-Cheek msimu huu lakini huenda ikakubali mchezaji huyo, 22, aliyeichezea Crystal Palace kuendelea kucheza kwa mkopo. (Mail)

Leicester City imewasilisha ombi la £12m ili kumnunua mchezaji wa Besikitas 29, Domagoj Vida, ambaye anaichezea Croatia katika kombe la dunia (Sabah, via Leicester Mercury)

Haki miliki ya picha Getty Images

Mada zinazohusiana