Tetesi za soka Ulaya Alhamisi 28.06.2018

Haki miliki ya picha Getty Images

Manchester United wako tayari kumsaini kipa wa klabu ya Stoke ,35, Lee Grant. Mchezaji huyo wa zamani wa kikosi cha Uingereza kisichozidi umri wa miaka 21 atatumika kama kipa wa ziada kwa David de Gea na Sergio Romero. (Telegraph)

Mchezaji wa klabu Everton na nahodha wa zamani wa Uingereza Wayne Rooney, 32, atatia saini mkataba wa miaka miwili na klabu ya DC United katika kipindi cha saa 36 . (Sky Sports)

Jorginho, Haki miliki ya picha Getty Images

Ajenti wa kiungo wa kati wa Napoli Jorginho, 26, anadai kwamba mchezaji huyo anakaribia kukamilisha uhamisho wake hadi Manchester City kwa dau la £43m . (Mirror)

Crystal Palace imempatia kocha Roy Hodgson kandarasi mpya ambayo itamweka katika klabu hiyo hadi 2020. (Sky Sports)

Mshambuliaji wa Croatia katika kombe la dunia Ante Rebic Haki miliki ya picha Getty Images

Everton inamnyatia mshambuliaji wa Croatia katika kombe la dunia Ante Rebic. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 anaichezea klabu ya Eintracht Frankfurt. (Mirror)

Southampton inakaribia kumsajili mshambuliaji wa basel na Norway Mohamed Elyounoussi, 23. (NBC)

kipa wa Manchester City Angus Gunn, Haki miliki ya picha Getty Images

Klabu hiyo pia ina hamu ya kumsajili kipa wa Manchester City Angus Gunn, 22, katika mkataba ambao unaweza kufika dau la £15m. (Mail)

Manchester City haitaangazia kifungu cha ununuzi cha kandarasi ya mchezaji wa Huddersfield raia wa Australia Aaron Mooy , 27 . (Manchester Evening News)

Kungo wa kati wa Argentina na West Ham Manuel Lanzini, Haki miliki ya picha Getty Images

Kungo wa kati wa Argentina na West Ham Manuel Lanzini, 25, anasema kuwa anatarajia kupona kutoka katika jeraha lake la goti kufikia mwanzo wa 2019. (Fox Sports)

Liverpool imemsajili mshambuliaji wa Uingereza wa timu ya vijana Bobby Duncan, 17, kutoka Manchester City. Duncan ni binamu wa aliyekuwa kiungo wa kati wa Liverpool Steven Gerrard. (Liverpool Echo)

Tetesi bora za Jumatano

Marco Asensio, Haki miliki ya picha Getty Images

Real Madrid inapanga kumuuza kiungo wa kati wa Uhispania Marco Asensio, 22, ili kutafuta fedha za kumnunua mshambuliaji wa PSG na Brazil Neymar, 26. Liverpool ina hamu ya kumsajili Asensio. (Sport - in Spanish)

Chelsea imewasilisha ombi la dau la £35m kumnunua beki wa Juventus Daniele Rugani, 23. Klabu hiyo inatumai kwamba raia huyo wa Itali atakuwa mchezaji wa kwanza kusajiliwa na mkufunzi Maurizio Sarri. (Evening Standard)

Haki miliki ya picha Getty Images

Kiungo wa kati wa Manchester United Marouane Fellaini atatoa tangazo kuhusu hatma yake mnamo tarehe mosi mwezi Julai. Raia huyo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 30 hajakubaliana na masharti ya klabu hiyo kuhusu mkataba mpya. (Manchester Evening News)

Jack Grealish, 22, yuko tayari kuondoka Aston Villa msimu huu ili kurudi katika ligi kuu ya Uingereza, huku Tottenham ikiongoza katika kutaka kumsajili mshambuliaji huyo wa Uingereza (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images

Arsenal inakaribia kumsaini beki wa Borussia Dortmund Sokratis Papastathopoulos, 30, huku ikiendelea na mazungumzo ya kutaka kumsajili beki wa Freiburg na Uturuki Caglar Soyuncu, 22. (Sky Sports)

Manchester United inamchunguza beki wa Itali na AC Milan Leonardo Bonucci, 31. (Yahoo)

Haki miliki ya picha Getty Images

Manchester City inatazama uwezekano wa kumsaini kiungo wa kati wa Australia Aaron Mooy, 27, kutoka Huddersfield . City pia ina mpango wa dau la £20m huku Everton, West Ham United na Southampton pia wakipanga kumnunua Mooy. (ESPN)

Haki miliki ya picha Getty Images

Liverpool itamchunguza mshambuliaji wake wa Ubelgiji Divock Origi ,23, katika kipindi cha wiki chache zijazo na kumpatia fursa kuonyesha umahiiri wake katika klabu hiyo. Origi alihudumu msimu uliopita akicheza kwa mkopo katika klabu ya Wolfsburg Ujerumani. (Liverpool Echo)

Wolves wamekataa ombi la dau la £12m kwa mshambuliaji wa Fulham na raia wa Ureno Ivan Cavaleiro, 24, (Sky Sports)

Haki miliki ya picha Getty Images

West Brom haimtaruhusu beki wa Uingereza Craig Dawson kuondoka katika klabu hiyo kwa gharama ya chini. Klabu hiyo ilikataa dau la £12m kutoka West Ham kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28. (Sky Sports)

Stoke City wanakaribia kuweka mkataba na winga wa West Brom na Jamhuri ya Ireland James McClean, 29, baada ya kuimarisha dau la kwanza la £4m bid. (Mail)

Haki miliki ya picha Getty Images

Mkufunzi wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola yuko tayari kumsaidia Marcelo Bielsa katika klabu ya Leeds kumpatia baadhi ya wachezaji wake kwa mkopo . (Sun)

Sporting Lisbon itamfuta kazi mkufunzi wake Sinisa Mihajlovic, siku chache tu baada ya kuajiriwa.(Record)

Mada zinazohusiana