Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 02.07.2018

Juan Quintero

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Juan Quintero

Wolves wamejaribu kumasaini kiungo wa kati wa Colombia Juan Quintero ambaye ameonyesha mchezo mzuri kwenye Kombe la Dunia nchini Urusi lakini wanakabiliwa na ushindani kutoka Real Madrid na Tottenham kwa mchezaji huyo wa miaka 25. (Mirror)

Chelsea wanamteua meneja mpya Maurizio Sari leo Jumatatu na mchezaji ambaye atamsaini kwanza ni kiungo wa kati wa Urusi Aleksandr Golovin, 22, ambaye atagharimu pauni milioni 27 kutoka CSKA Moscow. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Alassane Plea

West Ham na Fulham wanamenyana kwa pauni milioni 25 kumsaini mshambuliaji wa Nice Mfaransa Alassane Plea, 25. (Sun)

Newcasle pia nao wanammezea mate mshambuliaji wa zamani wa Lyon Plea, ambaye alifunga mabao 21 kwenye mashindano ya msimu uliopita. (Shields Gazette)

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Andros Townsend

Newcasle wanatathmini ofa kwa wing'a wa Crystal Palace muingereza Andros Townsend, 26, lakini ikiwa tu wataamua kumuuza wing'a msikochi Matt Ritchie, 28, kwenda Stoke City. (Telegraph)

Juventus wamekataa ofa ya Lazio ya pauni milioni 89 na kiungo wa kati wa Uruguay Rodrigo Bentancur, 21 kwa kiungo wa kati wa Serbia Sergej Milinkovic-Savic, 23. (Tuttosport - in Italian)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Matej Vydra

Matej Vydra anakaribia kuhamia Leeds kwa pauni milioni 11 baada ya mshambuliaji huyo wa miaka 26 kutolewa kutoka kambi wa mazoezi ya Derby huko Tenerife. (Telegraph)

Stuttgart hawatamuuza mlinzi mfaransa Benjamin Pavard, 22, kwa milioni euro 50 na wanataka kumweka mchezaji huyo kwa mwaka mwingine kulingana na mkurugenzi wa klabu hiyo ya Ujerumani. (Stuttgarter Nachrichten - in German)

Bora Kutoka Jumapili

Liverpool imeanza tena mazungumzo na Lyon kwa ajili ya kiungo mshambuliaji Nabil Fekir, 24. (Sunday Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Nabil Fekir

Lakini Manchester United pia inamuhitaji mchezaji huyo.(La Progres - via Sunday Express)

Chelsea inatarajia kumtangaza meneja wa zamani wa Napoli Maurizio Sarri kuwa meneja wao mpya juma lijalo. (Talksport)

Tottenham wanampango wa kumnyakua kiungo mshamuliaji wa River Plate na timu ya taifa ya Colombia, Juan Quintero, 25. (La Nueva - via 90min)

Leicester City wamemteua Jacques Bonnevay kuwa meneja msaidizi wakati Michael Appleton akiondoka. (Leicester Mercury)

Chanzo cha picha, Rex Features

Maelezo ya picha,

Michael Appleton

Mlinda mlango Thibaut Courtois yuko tayari kuondoka Chelsea ikiwa mbelgiji huyo atatimiza ndoto zake kuelekea Real Madrid. (Sunday Mirror)

The Blues wanasuka mipango ya kumnyakua mlina mlango wa Roma Alisson, 25 kwa kitita cha pauni milioni 65 wakiwa na mashaka ya kumpoteza Courtois. (Mail on Sunday)

Mlinda mlango wa Arsenal Petr Cech, 36, amesema Napoli imeonyesha kumuhitaji lakini yeye ana mpango wa kubaki Emirates. (Calcio Mercato)

Arsenal wanajiandaa kukamilisha mazungumzo kuhusu kumsajili kiungo mshambuliaji wa Uruguay Lucas Torreira, 22 kutoka Sampdoria juma lijalo. (Mail on Sunday)