Simu ya Putin ilichangia ushindi wa Urusi dhidi ya Uhispania?

Russia celebrate

Chanzo cha picha, Reuters

Maelezo ya picha,

Simu ya Putin ilichangia ushindi wa Urusi dhidi ya Uhispania?

Urusi ilipata uungwaji mkono wa Rais Vladimr Putin kabla ya mechi yao ya Kombe la Dunia ambapo ilipata ushindi dhidi ya Uhispania.

Putin alimpigia simu kocha wa Urusi Stanislav Cherchesov kabla ya Urusi kuwashinda mabingwa hao wa kombe la Dunia la mwaka 2010 kwa mikwaju wa penalti.

"Kabla ya mechi saa za mchana, Rais Putin alimpigia kocha simu na kumtakia mema," alisema msemaji wa Ikulu Dmitry Peskov alisema.

Putin hakuhudhuria mechi hiyo mjini Moscow na haijulikani ikiwa atahudhuria robo fainali ya Urusi.

Urusi wamefika kundi la timu nane za mwisho licha ya kuorodheshwa nambari 70 na Fifa katika viwango vya ubora wa soka duniani, ambalo ndilo taifa ya chini zaidi miongoni mwa timu zinazoshiriki.

Chanzo cha picha, AFP

Maelezo ya picha,

Ni mara ya kwanza kwa Urusi kufika robofainali Kombe la Dunia tangu kuvunjika kwa Muungano wa Usovieti

Walifuzu kutoka kundi lao kufuatia ushindi dhidi ya Saudi Arabia na Misri, kisha wakatoka sare ya 1-1 baada ya muda wa zaidi na kupata ushindi wa 4-3 kupitia penalti.

"Putin pia alisema licha ya matokeo yoyote na Uhisapnia, hakuna mtu nchini humo angewahukumu."

Urusi watakutana na Croatia kwenye mechi ya robofainali siku ya Jumamosi wiki hii.

Chanzo cha picha, EPA

Maelezo ya picha,

Mashabiki walijitokeza barabara za miji kusherehekea

Chanzo cha picha, Getty Images

Kikosi kamili cha Urusi

Walinda lango: Igor Akinfeev (CSKA Moscow), Vladimir Gabulov (Club Brugge), Andrey Lunev (Zenit St Petersburg).

Mabeki: Vladimir Granat, Fedor Kudryashov (both Rubin Kazan), Ilya Kutepov (Spartak Moscow), Andrey Semenov (Akhmat Grozny), Sergei Ignashevich, Mario Fernandes (both CSKA Moscow), Igor Smolnikov (Zenit St Petersburg).

Viungo wa kati: Yuri Gazinskiy (Krasnodar), Alexsandr Golovin, Alan Dzagoev (both CSKA Moscow), Aleksandr Erokhin, Yuri Zhirkov, Daler Kuzyaev (all Zenit St Petersburg), Roman Zobnin, Alexsandr Samedov (both Spartak Moscow), Anton Miranchuk (Lokomotiv Moscow), Denis Cheryshev (Villarreal).

Washambuliaji: Artem Dzyuba (Arsenal Tula), Aleksey Miranchuk (Lokomotiv Moscow), Fedor Smolov (Krasnodar).