Kombe la Dunia: Neymar aiondoa Mexico, Brazil yatua robo fainali

Neymar

Chanzo cha picha, Reuters

Neymar hakuchelea kung'ara kwenye mechi iliyotabiriwa kuwa na uwezo wa kukatiza maazimio ya Brazil kuliinua Kombe la Dunia mara yao ya 6 .

Nyota huyo amefanikiwa kuitingia timu yake Brazil 2-0 dhidi ya Mexico.

Mexico iliwatatiza mabeki wa Brazil Neymar hakuwa na uoga mbele ya lango na kila alipoona mwanya, alifyatua kombora.

Kufikia sasa Neymar ameandikisha shuti 23 dhidi ya wapinzani huku 12 mikwaju (12) ikizuiwa na wadakaji.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Willian apumzishwa baada ya uhodari dhidi ya Mexico.

Nyota huyo wa PSG pia ameonyesha ukarimu wake kwa wenzake kwa kubuni fursa 16, zaidi ya wafungaji wengine wote Kombe la Dunia kufikia sasa.

Mexico ilianza mchuano ikijaribu mbinu ilizotumia dhidi ya Ujerumani za kufunga goli la mapema na kukusanyana mbele ya lango lao.

Ushirikiano bora kati ya kipa wa Brazil Alisson Becker na walinzi wake Thiago Silva pamoja na Miranda ulikatiza mipango ya Carlos Vela na Javier Hernandez marufu Chicharito.

Licha ya timu zote kutekeleza uvamizi, pande hizo zilienda mapumziko bila kufungana.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Bao la Neymar

Kipindi cha Pili:

Brazil iliingia awamu ya pili kwa hamasa na kuhitaji tu dakika sita kuchukua uongozi.

Neymar, alijitengenezea nafasi nzuri karibu na lango na kuwa makini, punde tu baada ya mpira kuwavuka wote mbele ya lango, akiwemo kipa Ochoa, aliyezuia wafungaji wa Brazil, Neymar aliuwezesha mpira kufululiza na kutulia kwenye kamba.

Mexico iliwapa matumaini mashabiki wake kwa kufanya majaribio kwa lango la Brazil ili kusawazisha matokeo.

Vitisho vyao vilifanywa na Vela na Layun waliobadili njia na kuwaandama mabeki wa kulia na wa kushoto wa Brazil, Fagner na Filipe Luis.

Safu ya ufungaji ya Mexico ilipigwa jeki baada ya Kocha Juan Osorio kumtoa beki Rafael Márquez na kumtambulisha Miguel Layún.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Tumbo joto kwa kocha wa Mexico Juan Carlos Osorio

Mbinu zote za Mexico hazikuzaa matunda kwani Brazil ilitimua ushambulizi kama njia ya kujikinga na kuwadumisha Mexico eneo lao.

Bao moja la Brazil lilitenganisha pande hizo hadi dakika 10 za mwisho lakini kocha Tite hakusita kuzidisha nguvu za mabeki wake.

Mchezo wa Brazil ulibadilika wakati Fernandinho aliingia nafasi ya Paulinho. Kiungo huyo wa Manchester City, aliongeza ustadi wake kutuliza mechi.

Dakika chache baadaye, masaibu ya Mexico yaliongezeka baada ya Philippe Coutinho kumpisha Roberto Firmino.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Firmino

Nguvu mpya Firmino, alikamilisha mbio za Fernandinho na kuzamisha matumaini ya Mexico dakika mbili kabla ya muda wa kawaida wa mechi kukamilika. Ilikuwa ni mguso wake wa pili wa mpira.

Juhudi zake zimezua mjadala za iwapo Brazil inastahili kumuanzisha mbele ya Gabriel Jesus.

Iwapo atahamisha fomu yake nzuri ya Liverpool hadi timu ya taifa, mchango wako huenda ukawastawisha Coutinho na Willian.

Brazil itakwaruzana na mshindi kati ya Ubelgiji na Japan katika uwanja wa Kazan Arena, Kazan, siku ya Ijumaa.