Neymar ajitetea dhidi ya shutuma kuwa alimhadaa mwamuzi

Neymar ameshutumiwa kufanya udanganyifu uwanjani
Image caption Neymar ameshutumiwa kufanya udanganyifu uwanjani

Mshambuliaji wa Brazil Neymar amejitetea dhidi ya madai kuwa alimhadaa mwamuzi wakati timu yake ilipopambana na Mexico kwenye michuano ya kombe la dunia, akisema ''Ninasikia maumivu.''

Neymar,26, alimhadaa mwamuzi kuonyesha kuwa alitendewa vibaya sana na Miguel Layun wa Mexico anayedaiwa kumkanyaga kwenye kifundo cha mguu.

Kocha wa Mexico Juan Carlos Osorio alisema kitendo alichokiita cha ''kuigiza'' cha mchezaji huyo wa Paris St-Germain ''si mfano mzuri katika mchezo wa mpira wa miguu''.

Lakini Neymar alisema: ''Ni ngumu. Si kitu ambacho naweza kudhibiti''.

Neymar ameonekana kuudhi ulimwengu' kutokana na kitendo chake.

Lakini mwenyewe amesema: ''Nilikanyagwa isivyo haki. Sifikiri kama inapaswa kuwa hivyo.

''Ndio hivyo, waliongea sana kabla ya mchezo- na sasa wanakwenda nyumbani''.

Kejeli dhidi ya Neymar:

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Neymar amesema kuwa watu wana nia ya kumuangusha kimchezo

Neymar anakabiliwa na shutuma kuwa amekuwa akifanya udanganyifu kwenye michuano hii ya kombe la dunia.

Osorio amesema kuwa tukio lake na Layun lilidhoofisha kasi ya Mexico akimshutumu mwamuzi wa mchezo Gianluca Rocchi kuwa ''aliipendelea Brazil''.

''Ni aibu kwa mchezo wa soka, tulipoteza sana kwa sababu ya mchezaji mmoja,'' alisema meneja huyo baada ya kupoteza mchezo.

''Ni aibu kwa watu wote waliokuwa wakitazama, watoto wote wakitazama.Hakupaswi kuwa na kuigiza.Nafikiri tukio hili lina madhara kwa kasi na mtindo wa mchezo.

''Mchezo ulipendelea kabisa Brazil. Mwamuzi mara nyingi alikuwa akiingilia mchezo''.

Neymar kwa upande wake amesema hajali kukosolewa kwa kuwa anaona kuwa kunaweza kushusha ari ya mchezo, aliiambia TV Globo: ''Nafikiri zaidi ni jaribio la kunihujumu zaidi ya mengine yote''.

Kocha wa Brazil, Tite alimtetea mchezaji wake akisisitiza kuwa Layun ''alimkanyaga''.

''Niliona kwenye skrini,''alisema Tite.''Katika mechi iliyopita alifanya vizuri sana, na kwenye mchezo huu amecheza vizuri zaidi,'' aliongeza.

Neymar akaongeza: "Sijali kwa vyovyote vile ukosoaji huu, au sifa ninazomwagiwa, kwa sababu hilo linaweza kuathiri mtazamo. Katika mechi mbili zilizopita, sikuzungumza na wanahabari kwa sababu sikutana.

"Nahitaji tu kucheza, na kuwasaidia wachezaji wenzangu, na kuisaidia timu."

Mada zinazohusiana