Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 04.07.2018

Cristiano Ronaldo Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Cristiano Ronaldo

Juventus wana uhakika kuwa watamsaini mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo.

Mchezaji huyo wa umri wa miaka 33 ambaye ni nahodha wa Ureno yuko tayari kukubali mkataba wa pauni milioni 26 kwa mwaka. (Mirror)

Manchester City wako tayari kumsaini wing'a wa Leicester City raia wa Algeria Riyad Mahrez, 27, na kiungo wa kati raia wa Italia Jorginho, 26, kutoka Napoli kwa jumla ya pauni milioni 108. (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption William

Chelsea wanataka pauni milioni 70 kwa wing'a raia wa Brazil William wakati Barcelona na Manchester United wanamwinda mchezaji huyo wa umri wa miaka 29. (Mundo Deportivo)

Chelsea wamekataa ofa ya zaidi ya puani milioni 50 kwa William kutoka Barcelona. (Sky Sports)

Tottenham wanataka kumsaini kiungo wa kati mfaransa wa umri wa miaka 23 Adrien Rabiot, kutoka Paris St-Germain. (France Football)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Andre Gomes

Meneja wa Arsenal Unai Emery anataka kumsaini kiungo wa kati wa Barcelona Andre Gomes msimu huu. Mabingwa hao wa Uhispania wanataka pauni milioni 30 kwa mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Ureno. (Independent)

Kiungo wa kati wa Seveilla raia wa Ufaransa Steven N'Zonzi, 29, amekiambia klabu kuwa anataka kuondoka wakati Arsenal inaonyesha nia ya kumsaini. (Sun)

Mshambuliaji wa Chelsea raia wa Uhispania Alvaro Morata, 25, anaweza kutumiwa katika makubaliano ya kubadilishana wachezaji na mshambuliaji raia wa Argentina Gonzalo Higuain 30, kutoka Juventus. (Gazetta dello Sport - in Italian)

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Kasey Palmer

Derby County wamepewa ruhusa na Chelsea kuzungumzia kuhama kabisa kwa kiungo wa kati wa England Kasey Palmer, 21. (Sky Sports)

Manchester United wanakaribia kumsaini kiungo wa kati wa Lazio na Serbia Sergej Milinkovic-Savic, 23, wakati Juventus waliacha kumwinda.(Tuttosport via Manchester Evening News)

West Ham wanataka kumchukua mshambuliaji wa Napoli na Italia Roberto Inglese, 26, kwa mkopo. (Il Mattino via Football Italia)

Bora kutoka Jumanne

Itambidi mlinzi wa Uholanzi Daley Blind, mwenye miaka 28, apate kato la kipato ili kuweza kujiunga tena na Ajax kutoka Manchester United msimu huu wa joto. (Telegraph)

Huddersfield na Wolves wana hamu ya kumsajili winga wa Middlesbrough Adama Traore mwenye miaka 22. Mhispania huyo amefungwa kwa mkataba wenye thamani ya £ milioni 18m zinazohitajika ili aruhusiwe kuondoka. (Sun)

Kipa wa Leicester City na Denmark Kasper Schmeichel, atalengwa na Chelsea iwapo klabu hiyo itamuuza M'belgiji Thibaut Courtois, mwenye miaka 26, na Roma iwapo watamuuza mchezaji wa Brazil Alisson, 25. (Sky Sports)

Haki miliki ya picha EPA
Image caption Kipa wa Leicester City na Denmark Kasper Schmeichel akiokoa mkwaju

Napoli wameacha kumuwania mchezaji wa kiungo cha kati wa Italia na Manchester City Jorginho, mwenye miaka 26, kutoka orodha yake ya waliomo kwenye kambi yake ya mafunzo kabla kuanza kwa msimu. (Manchester Evening News)

Aliyekuwa kipa wa Juventus na Italia Gianluigi Buffon, mwenye miaka 40, anatarajiwa kusaini mkataba wa miaka miwili na mabingwa wa Ufaransa Paris St-Germain mwishoni mwa Juma. (L'Equipe)

Uhispania imemratibu aliyekuwa meneja wa Watford Quique Sanchez Flores kuwa meneja wake mpya baada ya kufutwa kwa Julen Lopetegui mkesha wa kuanza Kombe la Dunia kwa hatua ya kujiunga na Real Madrid. (AS)