Eric Abidal: Barcelona yakana rais wake wa zamani alimnunulia ini haramu beki wake

Eric Abidal Haki miliki ya picha AFP
Image caption Eric Abidal alishinda mataji manne ya ligi pamoja na mawili ya vilabu bingw Ulaya akiichezea Barcelona.

Abidal mwenye umri wa miaka 38, ambaye sasa ndio katibu wa klabu hiyo alifanyiwa upandikizaji baada ya uvimbe kupatikana katika ini lake.

Ripoti nchini Uhispania zinasema kuwa Sandro Rosell ambaye alikamatwa kwa ulanguzi wa fedha 2017, alinunua kiungo hicho.

Barcelona imekana kwa jumla kwamba hakuna makosa yaliofanyika katika swala hilo. Madai hayo pia yalipingwa na Abidal na kliniki ya Barcelona ambapo mchezaji huyo alifanyiwa upasuaji huo.

Barcelona iliongeza: Klabu hii imeshangazwa na ukali uliotumiwa kusambaza habari hii kuhusu swala nyeti.

Shirika la upandikizaji wa viungo vya ndani ya mwili nchini Uhispania limeanzisha uchunguzi wa ndani likishirikiana na hospitali husika na shirika la upandikizaji la eneo la Catalan.

Haki miliki ya picha David Ramos

Limesema kuwa habari iliopatikana inaonyesha ufadhili na upandikizaji ulikuwa kulingana na sheria zilizopo na itifaki za kliniki.

Abidal ambaye alihudumu kwa misimu sita katika klabu hiyo ya Nou Camp , alirudi kuichezea Barcelona mnamo mwezi Aprili 2013 kabla ya kujiunga na Monaco miezi mitatu baadaye.

Wiki iliopita mahakama ya Uhispania iliamuru kwamba Rosell , ambaye yuko kizuizini , atashtakiwa kwa mashataka ya ulanguzi wa fedha yanyohusisha uuzaji wa haki za runinga za mechi za Brazil.Barcelona imekana kwamba rais wake wa zamani Sandro Rosell alimnunulia ini aliyekuwa beki wa Ufaransa Eric Abidal kwa njia ya haramu.