Kombe la Dunia 2018 Brazil vs Belgium: Brazil kumkosa beki aliyejaza nafasi ya Dani Alves

Danilo Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Danilo amechezea Brazil mechi 19

Beki wa Brazil Danilo hatacheza tena Kombe la Dunia nchini Urusi baada yake kuumia kwenye kifundo cha mguu akifanya mazoezi Alhamisi.

Mchezaji huyo wa Manchester City aliumia mkesha wa mechi muhimu kwa Brazil robofainali Kombe la Dunia dhidi ya Ubelgiji.

Mechi hiyo itaanza saa tatu usiku saa za Afrika Mashariki katika uwanja wa Kazan Arena mjini Kazan.

Mchezaji huyo aliumia kwenye kano zilizo kwenye kifundo cha mguu wake wa kushoto.

Ingawa hatarajiwi kucheza tena, ameombwa kusalia na kikosi Urusi.

Danilo, 26, aliwachezea Brazil mechi moja pekee ambayo walitoka sare 1-1 na Uswizi mechi yao ya kwanza 17 Juni na kisha akaumia kwenye misuli ya paka.

Nafasi yake katika kikosi cha kuanza mechi Brazil imekuwa ikijajwa na beki wa kushoto anayechezea Corinthians, Fagner.

Danilo alikuwa ameitwa kwenye kikosi kujaza nafasi ya beki wa Paris St-Germain Dani Alves, ambaye alikosa michuano ya mwaka huu kutokana na jeraha la goti.

Kikosi cha Brazil kikoje?

Kiungo wa kati Casemiro amesimamishwa kucheza kutokana na kupata kadi mbili ya manjano na nafasi yake itachukuliwa na Fernandinho, kwa mujibu wa kocha wao Tite.

Beki wa kushoto Marcelo ambaye hakuwa sawa kabisa mechi yao ya mwisho amepona tatizo la mgomo na atachukua nafasi yake kutoka kwa Filipe Luis.

Winga Douglas Costa pia amepona jeraha la misuli.

Ubelgiji wakoje?

Belgium wanatumaini winga wao Adnan Januzaj atakuwa sawa kucheza baada yake kushindwa kuwachezea mechi yao iliyopita kutokana na jeraha ambalo halikufafanuliwa.

Kocha Roberto Martinez hana matatizo mengine ya majeraha.

Tathmini

Ubelgiji walitoka nyumba 2-0 mechi yao ya 16 bora dhidi ya Japan na kushinda 3-2, ambapo waliibuka kuwa timu ya kwanza Kombe la Dunia katika miaka 48 kutoka nyuma 2-0 na kushinda mechi.

Huenda ikawa vigumu hata hivyo kujikwamua dhidi ya Brazil iwapo watafungwa mabao kama hayo.

Brazil hufahamika kwa uchezaji wa kupendeza na kupiga chenga lakini wana matatizo safu ya ulinzi.

Hata hivyo wamefungwa bao moja pekee Urusi na hawajafungwa mechi 19 kati ya 25 walizocheza chini ya kocha wao wa sasa Tite.

Ubelgiji hata hivyo wana uwezo wa kutoa ushindani mkali kwa Brazil hasa kwa ufungaji.

Timu zote mbili zina wachezaji watatu waliokuwa wanashindania tuzo ya Ballon d'Or 2017; Neymar, Marcelo na Philippe Coutinho kwa Brazil, na Kevin de Bruyne, Eden Hazard na Dries Mertens kwa Belgium.

Wakufunzi wamesema nini?

Kocha wa Brazil Tite: "Itakuwa ni mechi kuu. Timu zote mbili zinafahamika kwa mchezo maridadi na wa kuvutia. Ubelgiji wana wachezaji wazuri na kocha mzuri pia. Nimekuwa kila wakati nawaweka kwenye kundi la wanaopigiwa upatu kushinda (Kombe la Dunia)."

Kocha wa Ubelgiji Roberto Martinez: "Tutahitaji nguvu. Ni lazima tujilinde vyema kadiri ya uwezo wetu na kuwaumiza tunapokuwa na mpira."

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ubelgiji wameshindwa mara moja pekee wakiwa na Roberto Martinez mechi yake ya kwanza nao Septemba 2016

Uwezekano wa Brazil kushinda Kombe la Dunia kwa mujibu wa watabiri umekuwa ukiimarika

Haki miliki ya picha Gracenote

Uwezekano wa Ubelgiji kushinda pia umeimarika

Haki miliki ya picha Gracenote

Takwimu Brazil v Belgium

  • Hii itakuwa mara ya tano kwa mataifa hayo mawili kukutana. Ya kwanza ilikuwa mechi ya kirafiki Brussels 1963 ambapo Ubelgiji walishinda 5-1 lakini Brazil walishinda mechi tatu zilizofuata.
  • Mara pekee walipokutana Kombe la Dunia ilikuwa ni katika raundi ya 16 mwaka 2002. Brazil walishinda 2-0 kupitia mabao ya kipindi cha pili yaliyofungwa na Rivaldo na Ronaldo na mwishowe walishinda michuano hiyo.

Wachezaji

Brazil

Walinda lango: Alisson (Roma), Ederson (Manchester City), Cassio (Corinthians).

Mabeki: Danilo (Manchester City), Fagner (Corinthians), Marcelo (Real Madrid), Filipe Luis (Atletico Madrid), Thiago Silva, Marquinhos (both Paris St-Germain), Miranda (Inter Milan) Pedro Geromel (Gremio).

Viungo wa kati: Casemiro (Real Madrid), Fernandinho (Manchester City), Paulinho (Barcelona), Fred (Shakhtar Donetsk), Renato Augusto (Beijing Guoan), Philippe Coutinho (Barcelona), Willian (Chelsea), Douglas Costa (Juventus).

Washambuliaji: Neymar Jr (Paris St-Germain), Taison (Shakhtar Donetsk), Gabriel Jesus (Manchester City), Roberto Firmino (Liverpool).

Ubelgiji

Walinda lango: Koen Casteels (Wolfsburg), Thibaut Courtois (Chelsea), Simon Mignolet (Liverpool).

Mabeki: Toby Alderweireld (Tottenham Hotspur), Dedryck Boyata (Celtic), Vincent Kompany (Manchester City), Thomas Meunier (Paris St-Germain), Thomas Vermaelen (Barcelona), Jan Vertonghen (Tottenham Hotspur).

Viungo wa kati: Yannick Carrasco (Dalian Yifang), Kevin de Bruyne (Manchester City), Mousa Dembele (Tottenham Hotspur), Leander Dendoncker (Anderlecht), Marouane Fellaini (Manchester United), Eden Hazard (Chelsea), Thorgan Hazard (Borussia Monchengladbach), Adnan Januzaj (Real Sociedad), Dries Mertens (Napoli), Youri Tielemans (Monaco), Axel Witsel (Tianjin Quanjian).

Washambuliaji: Michy Batshuayi (Chelsea), Nacer Chadli (West Brom), Romelu Lukaku (Manchester United).

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii