Tetesi za soka Ulaya Jumamosi 07.07.2018

Ronaldo

Chanzo cha picha, Getty Images

Real Madrid inamtaka mshambuliaji wake Cristiano Ronaldo kuwaambia mashabiki wa klabu hiyo kwamba hajalazimishwa kuondoka katika klabu hiyo iwapo mchezaji huyo wa Ureno ataelekea Juventus.. (Mail)

Manchester United inataka kumsaini upya mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 lakini wameambiwa kwamba kumekuwa na mazungumzo mazuri kuhusu uhamisho wake kuelekea Juve. (Independent)

Chanzo cha picha, Getty Images

Paris St-Germain iko tayari kulipa dau la £100m ili kumnunua kiungo wa kati wa Chelsea na Ufaransa N'Golo Kante, 27. (Goal)

West Ham iko tayari kumruhusu mshambuliaji wa Ufaransa na Marseille Dimitri Payet kurudi mjini London iwapo atakubali kupunguza mshahara wake.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 31 aliondoka katika klabu hiyo akiwa amekasirika yapata miezi 18 iliopita. (Mirror)

Chanzo cha picha, Getty Images

Jack Wilshere amefanya ukaguzi wa matibabu katika klabu ya West Ham huku klabu hiyo ikitaka kumsajili kiungo huyo aliye huru kwa kandarasi ya miaka mitatu na mapato ya £5m. (Times - subscription required)

Winga wa Crystal Palace Wilfried Zaha amekataa ombi la kumpatia mshahara wa £120,000 kwa wiki katika klabu hiyo.

Chanzo cha picha, Getty Images

Tottenham, Everton na Borussia Dortmund wameripotiwa kuwa na hamu ya kumsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 kutoka Ivory Coast. (Sun)

Manchester United wamewaorodhesha mabeki wanane ambao inataka kuwanunua na watalazimika kulipa dau la kuvunja rekodi ili kuwa na fursa ya kuwasajili baadhi yao.. (Express)

Chanzo cha picha, Getty Images

Arsenal imeanzisha mazungumzo na kiungo wa kati wa Sevilla na Ufaransa Steven N'Zonzi. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 awali aliichezea Blackburn na Stoke. (Sky Sports)

Chanzo cha picha, Getty Images

Everton wameonyesha hamu yao katika kumsajili mshambulikaji wa Barcelona na Uhispania Paco Alcacer, 24. (Sport)

Kiungo wa kati wa Southampton na Uholanzi Jordy Clasie, 27, yuko tayari kurudi katika klabu yake ya zamani Feyenoord. (Sun)

Chanzo cha picha, Getty Images

Saint-Etienne wameimarisha ombi lao la mshambuliaji wa Sunderland na Tunisia Wahbi Khazri, 27, licha ya ushindani mkali kutoka kwa klabu ya Ligue 1 Rennes. (L'Equipe - in French)

Kiungo wa kati wa Sunderland Yann M'Vila, 28, huenda akarudi Uingereza.

Huduma za raia huyo wa Ufaransa ambaye anaichezea Saint-Etienne, zinahitajika na klabu za Fulham na Crystal Palace. (Talksport)

Chanzo cha picha, Getty Images

Wolves imewasilisha dau la kuvunja rekodi la £16m kwa winga wa Manchester City na Ukraine Oleksandr Zinchenko, 21. (Sky Sports)

Kiungo wa kati Arthur Melo, 21, ametangaza anaihama klabu ya Brazil Gremio ili kujiunga na Barcelona mara moja, huku mabingwa hao wa Uhispania wakipanga kumnunua (Reuters)

Chanzo cha picha, Getty Images

Mmiliki wa klabu ya Aston Villa Tony Xia amesema kuwa anamuunga mkono mkufunzi Steve Bruce ijapokuwa wachezaji watalazimika kuuzwa ili kuafikia masharti ya kifedha ya Fifa ya fair Play. (Mirror)

Ryan Giggs, Robbie Keane, Damien Duff, Paul Scholes na Rio Ferdinand ni miongoni mwa baadhi ya wachezaji wa zamani ambao watashiriki katika mechi ya kutoa heshima kwa kiungo wa kati wa zamani wa klabu za Celtic, Manchester United na Sunderland Liam Miller, aliyefariki akiwa na umri wa miaka 36 mwezi Februari. (Mail)