Tetesi za Soka Ulaya Jumatatu 09.07.2018

Eden Hazard Haki miliki ya picha PA
Image caption Eden Hazard

Rais wa Real Madrid Florentino Perez anaripotiwa kuwa tayari amechagua namba ya Eden Hazard ikiwa mchezaji huyo wa Chelsea na Ubegiji atahamia Barnabau. (Diario Gol via Star)

Nduguye Antonio Conte amedai kuwa meneja huyo mwenye miaka 48 raia wa Italia atabakia Chelsea msimu unaokuja, licha ya kuwepo uvumi kuhusu hatma yake. (Mirror)

Haki miliki ya picha Rex Features
Image caption Riyad Mahrez

Manchester City wameafikia makubaliano ya pauni milioni 60 na Leicester kumsaini Riyad Mahrez huku mchezaji huyo wa umri wa miaka 27 akitarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kiafya ndani ya saa 48 zinazokuja. (Mail)

Arsenal wako kwenye mazungumzo na Loriet kuhusu kusainiwa kwa mchezaji huyo wa miaka 19 mfaransa, wa kikosi cha walio chini ya miaka 20 Matteo Guendouzi, (Sky Sports)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Lucas Torreira

Kiungo wa kati wa Uruguay Lucas Torreira 22 ambaye anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kiafya huko Arsenal leo Jumatatu kabla ya kuhama kwake anasema anataka kupata fursa kubwa. (Metro)

Baba yake Mesut Ozil amemtaka kiungo wa kati wa Arsenal kumaliza taaluma yake na Ujerumani baada ya mchezaji huyo wa miaka 29 kulaumiwa kufuatia matokeo mabaya kwenye Kombe la Dunia. (Bild via Talksport)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Frank Lampard

Meneja mpya wa Derby Frank Lampard amekuja na ofa ya mwisho kwa mlinzi wa West Ham Reece Burke huku mchezaji huyo wa miaka 21 akitarajiwa kuhamia Hull City. (Sun)

Meneja wa Ajax Erik ten Hag amethibitisha kuwa klabu inataka tena kumsaini mlinzi wa Manchester United Daley Blind, 28, ambaye alikuwa na wakati mgumu kuonyesha uwezo wake huko Old Trafford. (Sky Sports)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mario Balotelli

Mshambuliaji raia wa Italia Mario Balotelli yuko huko Marseille ili kuweza kukamilisha kuhama kwake. Mchezaji huyo wa zamani wa Nice na Manchester City ametembelea kambi ya mazoezi ya klabu huyo wakati mazungumzo ya mkataka yakiendelea. (RMC Sport)

Meneja wa Middlesbrough Tony Pulis analenga kumsaini mshambuliaji wa Burnley Sam Vokes, 28, lakini Britt Assombalonga, 25, huenda yuko njiani kuihama klabu hiyo. (Northern Echo)

Liverpool hawana nia ya kumsaini kiungo wa kati wa Aston Villa Jack Grealish wakati mchezaji huyo wa miaka 21 akihusishwa na kuhama kutoka Villa Park. (Liverpool Echo)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Aston Villa

Lakini klabu hiyo wa Anfield imepokea ofa za mikopo kutoka Norwich na Sheffield United kwa mchezaji wa miaka 18 mshambuliaji Ben Woodburn. (Goal)

Aliyekuwa mlinzi wa zamani wa Aston Villa na Cardiff Kieran Richardson, 33, anafanya mazoezi na West Brom akipanga kurudi kwennye kandanda baada ya miezi 18 nje. (Birmingham Mail)

Mlinzi wa Nice Jean-Michael Seri ameonekana huko London wakati Chelsea, Arsenal na Fulham wakiwa na nia ya kumsaini mchezaji huyo wa miaka 26 raia wa Ivory Coast. (Star)

Bora kutoka Jumapili

West Ham wametoa ofa ya pauni milioni 17.5 kwa mshaabulizi wa Borussia Dortmund raia wa Ukraine Andriy Yarmolenko, 28 ambaye alijiunga na klabu hiyo ya Ujerumani mwaka uliopita kwa kima cha pauni milioni 23. (Sky Sports)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Andriy Yarmolenko

West Ham pia wanatarajiwa kumaliza mpango wa kumwinda aliyekuwa kiungo wa kati wa Arsenal na England Jack Wilshere, 26, ambaye sasa hana mkataba siku ya Jumatatu. (Mirror)

Image caption Jack Wilshere

Rais wa Lyon Jean-Michel Aulas bado anaamini kuwa kiungo wa kati wa Ufaransa Nabil Fekir atakuwa kwenye orodha ya klabu hiyo msimu ujao baada wa mpango wake wa kujiunga na Liverpool kufanikiwa. (Goal)

Manchester United wana uhakika wa kumsaini mshambulizi wa Chelsea William , 29, wakati ambapo sasa Brazil wako nje ya Kombe la Dunia. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption William

Lakini nyota wa Barcelona Lionel Messi huenda akazuia William kuelekea Manchester United, kwa kuwa Messi anataka kuungana na mchezajihuyo mwenye miaka 28 huko Nou Camp. (Manchester Evening News)