Zlatko Dalic: Kama tulimzuia Messi hata Kane tutamzuia

Ivan Rakitic tackles Barcelona club mate Lionel Messi as Croatia beat Argentina in the World Cup Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Croatia waliwashinda Argentina 3-0

Kocha wa Croatia Zlatko Dalic amesema kuwa kikosi chake tayari kimefanikiwa kumzuia Messi hivyo kinaweza kumkabilia Harry Kane Jumatano katika nusu fainali.

Timu hizo zinakutana mjini Moscow kushindania nafasi ya fainali ya tarehe 15 Julai baada ya upande wa Dalic kuwatimua Urusi siku ya Jumamosi.

Dalic aliwataja Kane na Raheen kama tisho kwenye timu ambayo haina udhaifu.

"Lakini tunaamini uwezo wetu, alisema. "Hatuwaogopi England."

"Kane ni mfungajia bora- sio rahisi kumzuia. Lakini tuna mabeki wa kati. Tulifanikiwa kumzuia Messi na [Christian] Eriksen kwa hivyo tuna matumaini ya kumzuia Kane."

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Zlatko Dalic

Kutokana na kukosa kufunga akiwa na jesi ya England kwa karibu miaka mitatu, mshambuliaji wa Manchester City Sterling amekosolewa na baadhi wa wafuasi.

Hata hivyo wachezaji na Manchester United David Beckham na Gary Neville wamemuunga mkono mchezaji huyo wa miaka 23 na Dalic naye anamtaja kuwa mchezaji mzuri.

Kocha huyo wa miaka 51 ambaye ameiongoza timu hiyo ya taifa tangu Oktoba aliulizwa kuhusu uwezo wa England na pia udhaifu na akasema "siwezi kusema kuna udhaifu, wako nusu fainali, hilo tu linasema kila kitu.

"Walionyesha kutoka kwa michezo ambayo nimeitazama kuwa wanacheza mpira na wana mbio sana.

"Nafikiri kuwa Raheen Sterling ni mchezaji muhimu kwa sababu naa mbio sana na akiungana na Harry Kane ni hatari sana."

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Vida ambaye alifunga bao muda wa ziada aliepuka marufuku ya Fifa

Aliendelea kuisifu kazi yake Sterling akisema makocha wake watakuwa wakiichambua kikosi hicho cha Gareth Southgate kwa karibu siku mbili zinazokuja.

"Waliwashinda Sweden kwa njia rahisi kwa hivyo tunajua kuwa watakuwa washindani wagumu na tunawaheshimu," aliendelea kusema.

Kulikuwa na nafuu katika kikosi cha Croatia baada ya mlinzi Domagoj Vida kuonywa na Fifa na kuepuka marufuku, kwa kuonekana akiipongeza Ukrain wakati wa ushindi wao dhidi ya Urusi kwenye video moja ya mtandao.

Vida ambaye alifunga bao muda wa ziada kabla ya ushindi wa timu yake dhidi ya Urusi kwa mikwaju ya penalti alisema kwa sauti "Utukufu kwa Ukraine," kwa lugha ya Ukaine

Vida baadaye alisema alikuwa anafanya mzaha, "ushindi huo ulikuwa kwa Croatia, hakuna siasa."