Urafiki kugeuka uhasimu, nusu fainali Ufaransa v Ubelgiji

Ufaransa Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kikosi cha Ufaransa mazoezini

Kipute hicho kimepachikwa jina ''mkwaruzano wa marafiki.'' Mechi ya leo inawakutanisha mabingwa wa dunia 1998 dhidi ya 'kizazi cha dhahabu' cha Ubelgiji.

Pande zote zilipigiwa upatu kuliinua Kombe, lakini ni mmoja kati yao atatua fainali, siku ya Jumapili, Moscow.

Mshindi atakwatuana na Croatia au Uingereza - watakaochuana Jumatano - lakini kwanza, nani atapenya?

Ufaransa v Ubelgiji

Uwepo wa kina Romelu Lukaku, Eden Hazard, Kevin de Bruyne, Antoine Griezmann, Kylian Mbappe na Paul Pogba, kwenye safu za timu hizi, zimewawezesha kujigamba kuwa na washambuliaji wa kuogopewa duniani.

Lakini ni wakufunzi wao wanaotumia uwezo wa wachezaji hawa kulingana na mahitaji.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Romelu Lukaku

Meneja wa Ufaransa Didier Deschamps - anayenuia kuinua Kombe akiwa meneja baada ya kufanya hivyo akiwa mchezaji, analenga kuwafikia waliofanikiwa kiwango hicho- Mario Zagallo na Franz Beckenbauer - ameshtumiwa kwa kutotumia vizuri nguvu za kikosi chake.

Lakini kufikia sasa, siri ya Ufanisi wa Ufaransa Urusi imekuwa juhudi, na sio uhodari ilivyotarajiwa.

Bao la kuchelewa mechi yake ya kwanza, iliiwezesha kuifunga Australia, baadaye ikainyuka Peru 1-0 mechi yake ya pili, na kutoka sare ya kutofungana na ya kuudhi dhidi ya Denmark.

Ingawa walivutia zaidi kwa kuiduwaza Argentina 4-3 mechi ya mchujo, sio kulingana na mbinu za Deschamps.

"Ikiwa unasaka ushindi wa 5-0, usije Kombe la Dunia, hili hulipati," alisema.

Licha ya Deschamps kutozungumziwa vizuri, Martinez wa Ubelgiji amejizolea sifa kochokocho.

Licha ya Usajili usiotarajiwa, miezi mitatu tu baada ya kupigwa kalamu na klabu ya Everton, amekuwa na mchango mkubwa.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Kylian Mbappe

Hajawahi kufungwa mechi muhimu tangu achukue usukani na kuwa mkufunzi wa Ubelgiji.

Ngarambe yake ya mwisho kufungwa ilikuwa akiwa meneja wa Everton, mechi ya kirafiki waliyolazwa 3-0 na Sunderland, Mei 2016.

Hata hivyo, Martinez ameipa Ubelgiji ushindi mechi 19 na kutoka sare mechi 5 ikiwemo ule wa 2-1 dhidi ya Brazil katika robo fainali.

Mabao 14 ya Ubelgiji Kombe la Dunia ndio mengi zaidi kufungwa kiwango hiki tangu safari ya Brazil mnamo 2002 ya Kulitwaa taji walipofunga magoli 15.

Kipindi cha kazi kwa kizazi cha dhahabu cha Ubelgiji.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Eden Hazard

Uingereza inafahamu Zaidi kuhusu 'kizazi cha dhahabu' cha wachezaji

Kizazi chao hakijabeba Kombe lolote la kimataifa, lakini cha Ubelgiji kimeonyesha dalili za kuondoka na tuzo bora zaidi ya yote.

Red Devils wameondoka na ushindi mechi yao yote ya makundi na kuipiga Japan 3-2 kwa kutoka nyuma 2-0 kabla ya kufunga kazi kwa kuwadhalilisha mabingwa mara 5 wa dunia, Brazil 2-1 kwenye robo-fainali.

Ubelgiji ililelemewa hatua ya robo fainali kwenye Kombe la Dunia 2014 na Kombe la mataifa bora Ulaya 2016.

Muda unayoyoma kwa nyota hao?

"Ni muhimu kila mmoja kuelewa kuwa Ubelgiji ina idadi ya watu milioni 11 na wachezaji wa sasa hawakuchipuka tu ghafla kwa bahati," alizidi Martinez. "Kuna mfumo wa kitaalam ndani ya soka ya Ubelgiji.Ni taifa lililomakinika kuboresha vipaji vyake vya soka.

Mfaransa Henry ajiandaa kuwaliza wafaransa

Thierry Henry alizaliwa karibu na mji wa Paris na ameifungia Ufaransa mabao 53 katika mechi 123 pamoja na kushinda Kombe la Dunia 1998 na lile la Euro 2000.

Lakini sasa ni mmoja wa wale wanaolenga kuiangamiza Ufaransa nchini Urusi akiwa naibu meneja wa Ubelgiji.

"Thierry Henry ana umuhimu mkubwa kwetu," alinukuliwa beki Toby Alderweireld. "Yeye hutusimulia kuhusu enzi zake akicheza na simulizi hizo hutumotisha.

"Asemalo, huishia kuwa muhimu sana lenye kutufaa. Uwepo wake, uzoefu wake Kombe la Dunia,yote yana mchango chanya."

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Thierry Henry

Mechi ya leo inamkutanisha na mchezaji mwenzake wa zamani, Deschamps. Wawili ha hawajawahi kufungwa mechi 21 walizoiwakilisha Ufaransa.

Deschamps alisema: "Linashangaza kumuona upande wa Ubelgiji ilihali ni Mfaransa. Ni mtu ninayemuenzi na namtakia kila la heri."

Kiungo wa Ubelgiji, De Bruyne ana uhakika Henry "anataka waibuke bora kuliko Ufaransa" - lakini mkabaji wa Ufaransa Lucas Hernandez anafikiria kuwa, licha ya matokeo, itakuwa ni ushindi kwa Henry, mfungaji wa zamani wa Arsenal na Barcelona.

"Ufaransa inajuwa ni shujaa wake na inamfahamu alikuwa mchezaji mzuri," alisema Hernandez.

"Lakini tukishinda, atafurahia kwani ni Mfaransa."

'Uhasimu wa kirafiki'

Mechi hii itakuwa ni ya kwanza kati ya mataifa yenye mipaka yanayokaribiana tangu 1986 Ujerumani magharibi, ilipoonana na Ufaransa.

Kiungo matata wa Ubelgiji, Hazard alizaliwa karibu na mpaka wa Ufaransa,huku jarida la Le Soir likimtaja kuwa "Mfaransa Zaidi ya Wabelgiji wote". Picha iliyosambzwa mtandaoni inaonyesha Hazard na nduguye wakiwa wamevaa sare za Ufaransa.

Wenyeji katika kijiji cha Warneton, katikatiki ya mpaka, hawajui watamshabikia nani.

Antoine Griezmann v Romelu Lukaku

Shindano lingine, kipindi kingine Griezmann amenawiri kwa Ufaransa. Mfungaji huyo wa Atletico Madrid alifunga mabao 6 shindano la Euro 2016 na kunyakua kiatu cha dhahabu huku timu yake ikimaliza ya pili baada ya kufungwa na Ureno kwenye fainali.

Griezmann amesajili mabao matatu kufikia sasa nchini Urusi, moja nyuma ya Lukaku.

Mfungaji wa Uingereza Harry Kane anaongoza akiwa na mabao 6.

Kylian Mbappe v Eden Hazard

Chipukizi Mbappe alijitambulisha Jukwaa la Kombe la Dunia kwa kuonyesaha mchezo wa hali ya juu walipoitawala Argentina 4-3 hatua ya mchujo.

Staa huyu wa Paris St-Germain aling'aa na kuvutia sifa nyingi mechi hiyo kupitia kasi yake na umahiri wake mbele ya wavu ambapo alitandika mabao mawili.

Hapo awali, goli lake dhidi ya Peru - ambalo alifunga akiwa na miaka 19 na siku 183 - lilimfanya mchezaji mwenye umri mdogo kuifungia Ufaransa kwenye shindano la kimataifa.

Kwingineko, nahodha wa Ubelgiji Hazard, tayari amejipa mabao mawili na kuchangia ufungaji wa mengine mawili.

Wachezaji wote wanapenda kukimbia washikapo mpira na kati ya wale waliosalia kwenye Kombe la Dunia, Mbappe (37) na Hazard (30) ndio wanaoongoza kwa idadi ya chenga kamili kufikia sasa.

"Akiwa mdogo alikuwa akitazama video zangu, " Hazard aliiambia RMC Sport. "Kwa sasa, ni kinyume, Ninaheshimu sana mafanikio yake katika umri wake."

Paul Pogba v Kevin de Bruyne

Uwaniaji wa ubabe katikati kati ya majimbi ya Manchester.

Pogba wa United na De Bruyne wa City watakuwa wanasaka kupimana nguvu huku kila mmoja akilenga kuvuta ngoma upande wake na kuisaidia timu yake.

Takwimu zinaonyesha kuwa De Bruyne ndiye amebuni fursa nyingi kwa wenzake yaani mara tatu Zaidi ya mchangoi wa Pogba, lakini nguvu za Pogba zipo kwenye ukabaji kuliko usamblizi.