Mashabiki wengi wa michuano ya kombe la dunia 2018 wanashindwa kutofautisha rangi

Mamilioni ya watu duniani wana tatizo la upofu rangi Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mamilioni ya watu duniani wana tatizo la upofu rangi

Sean Hargrave anasema anapenda mpira wa miguu kupita kiasi lakini alipokaa na kutazama mechi ya ufunguzi ya kombe la dunia mwaka 2018 hakuweza kutofautisha timu zilizokuwa zikicheza.

Watu milioni 320 duniani wana tatizo la upofu rangi.Takwimu zinasema kuwa hali hii inamtokea mchezaji mmoja katika kila timu ya mpira wa miguu, na karibu nusu ya dunia waliokisiwa kutazama michuano ya kombe la dunia, wengi wao wanaghadhabu na waanaaji, Fifa kwa kushindwa kuchukua hatua.

Watu wenye upofu rangi hawawezi kutofautisha kati ya rangi zifuatazo:

Nyekundu, rangi ya machungwa, kijani na kahawia

Nyekundu na nyeusi

Buluu,zambarau na pinki iliyokolea

Senegal na Colombia walicheza wakiwa wamevaa rangi za kijanina manjano, rangi zilizowachanganya baadhi ya mashabiki, vivyo hivyo ilitokea kwa England na Sweden, ambapo mashabiki walishindwa kutofautisha rangi ya limao aliyokuwa amevaa mlinda mlango wa England Jordan Pickford na ukilinganisha na ya machungwa ya mlinda mlango wa Sweeden.

Haki miliki ya picha ASTON VILLA FOOTBALL CLUB
Image caption Katy Moran wa tiku ya Aston Villa ya wanawake amesema anapata tabu kutazama rangi na kubaini nani ni nani

Katy Moran, 27 ambaye ana shida ya upofu rangi na anayechezea Aston Villa ya wanawake ameiambia BBC kuwa wakati mwingine huangalia soksi ili kutambua nani ni nani anapokuwa uwanjani mwenyewe.

''Msimu uliopita tulicheza na Millwall.Villa walivaa nyekundu iliyoiva(damu ya mzee) na Millwall walikuwa wamevaa kama blue nyeusi.Waliingia uwanjani nikawaza peke yangu, afadhali sichezi, na timu zote zilivaa kaptula nyeupe.

Mwonekano wa wachezaji uliharibu mchezo wake . ''Unakazana kubaini nani ni nani.Ningekuwa mimi nacheza (Millwall) uchezaji wangu, nisingekuwa na maamuzi ya haraka, kwa sababu siwezi kufikiri haraka kama mchezaji wangu anakwenda kuchukua mpira, au napaswa kumsaidia

''kuna wakati tulikuwa tunacheza na nikatoka nje ya eneo kwa sababu sikuwa ninafahamu wako wapi.Nilikuwa nakimbiakimbia na wakawa wananiuliuza, ''unakwenda wapi?!''

Haya ni matatizo ambayo wachezaji wanayapata ikiwemo kwenye michuano ya kombe la dunia.

Dakika chache kabla ya kukutana na timu ya kimataifa ya Denmark kuanza safari ya kwenda Urusi, kiungo wa kati Thomas Delaney alipiga simu kwenye kituo cha redio kumuunga mkono mtu aliyekuwa na tatizo la upofu rangiambaye alisema alikuwa anapata tabu kutenganisha Denmark na Mexico katika mechi ya kirafiki kuelekea Kombe la dunia.

Akijitambulisha kwa jina la ''Thomas'' Delaney alikiambia kituo hicho kuwa :'' Mimi ni na upofu rangi hasa kwenye rangi nyekundu-kijani ambayo siwezi ikusema ni mbaya sana huwa inatokea.Siku moja iliniwia ngumu uwanjani kujua nani yuko kwenye timu yangu nani yuko timu nyingine.

Kathyrn Albany-Ward, mwanzilishi wa taasisi inayotoa elimu kuhusu tatizo la upofu rangi, amesema Dane ni mchezaji wa kwanza ambaye amezungumza kwa uwazi kuhusu changamoto anayokabiliana nayo ''sidhani kama anafahamu kama nijambo kubwa sana alilolifanya la kusema ukweli''. Alieleza.

Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Thomas Delaney wa Denmark anayekipiga Borussia Dortmund alikiambia kituo cha redio cha told the radio DR P3 kuwa alitaka kumwambia mpiga simu aliyetangulia kuwa si yeye pake yake mwenye upofu rangi

''Watu wengi hawazungumzi kwa kuwa wana hofu kuwa itaathiri thamani yao:iwapo watacheza au kukaa kwenye benchi, hicho ndicho wanachokihofia''.

Uoga unaeleweka, hasa kutokana na mashabiki kuchukulia kila udhaifu unaojionyesha.''Ile haikuwa kadi nyekundu, mwamuzi lazima ana upofu rangi!''.

Mitandao ya kijamii imetoa nafasi kwa mashabiki wa mpira wa miguu wenye upofu rangi kuelezea namna hali hiyo ilivyowasumbua

Taasisi inayotoa elimu kuhusu upofu rangi imekuwa ikifanyia uhakiki uwanja ambao utatumika kwenye michuano ya Uefa mwaka 2020 na kubainisha vitu mbalimbali ambavyo rangi zake zitaweza kutambulika kirahisi kama vile rangi za alama za njia za kutokea, alama za usalama na alama za maelekezo mengine kuhakikisha zinaonekana vizuri kwa watu wenye shida ya kutotofautisha rangi

Baadhi ya klabu za Uingereza pia zinafanya jitihada hizo hizo.Tottenham Hotspur imebuni tovuti yake na tiketi za msimu zisizo na rangi zenye kukanganya kwa mashabiki wake hasa wale wanaotumia rangi kubaini nafasi zao za viti uwanjani.