Croatia yaichapa England 2-1, yatinga fainali kombe la dunia kwa mara ya kwanza

Croatia watacheza na Ufaransa katika fainali ya Jumapili
Image caption Croatia watacheza na Ufaransa katika fainali ya Jumapili

Croatia wameingia fainali za kombe la dunia kwa mara ya kwanza katika historia, baada ya kuichapa England 2-1 katika mchezo ambao ulichezwa kwa dakika 120.

England ilianza kujipatia goli kupitia kwa Kieran Trippier dakika ya tano baada ya kupiga mkwaju wa adhabu ndogo uliokwenda moja kwa moja nyavuni.

Kipindi cha kwanza kiliisha kwa England kwenda mapumzikoni ikiwa kifua mbele.

Image caption Wachezaji wa England wakifarijiana baada ya mchezo

Kipindi cha pili Croatia ilitumia muda mwingi kumiliki mpira na kufanikiwa kusawazisha kupitia kwa Ivan Perisic aliyeonyesha kandanda safi na kuwa nyota wa mchezo.

Ufaransa watua fainali ya Kombe la Dunia Urusi

Mfahamu Samuel Umtiti aliyewafikisha Ufaransa fainali Kombe la Dunia

Goli hilo liliupeleka mchezo huo dakika 30 za nyongeza huku kila timu ikicheza kwa tahadhari ya hali ya juu.

Image caption Luka Modric akipongezwa na meneja wa England Gareth Southgate baada ya mchezo

Hatimaye mshambuliaji wa Juventus ya Italia Mario Mandzukic akaandika goli la pili na la ushindi kwa Croatia na hivyo kutinga fainali itakayochezwa dhidi ya Ufaransa katika uwanja wa Luzhniki mjini Moscow Julai 15.

England itacheza na Ubelgiji katika mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu Julai 14.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii