Kombe la Dunia 2018 Croatia 1-2 England: Mashabiki walivyosherehekea kuwashinda England nusufainali, London 'walivyoomboleza'

Croatia's supporters celebrate a goal as they watch Croatia -V-England at the main square in Zagreb Haki miliki ya picha AFP/Getty Images
Image caption Mashabiki wakisherehekea Zagreb

Mashabiki wa Croatia walisherehekea usiku kucha baada ya taifa lao kuwaondoa England kutoka kwa michuano ya Kombe la Dunia Urusi na kufuzu kwa fainali kwa mara yao ya kwanza kabisa, England waliomboleza.

Croatia walipata ushindi wa 2-1 baada ya mechi kumalizika sare ya 1-1 muda wa ziada.

Mashabiki walijaza uwanja ulio katikati mwa mji mkuu wa Croatia wa Zagreb wakiimba na kupeperusha bendera za taifa hilo. Baadhi walijitumbukiza hadi kwenye chemchemi za maji zinazopamba uwanja huo.

Mabao yalivyofungwa

Kieran Trippier dakika ya 5 Croatia 0-1 England

Ivan Perisic dakika ya 68 Croatia 1-1 England

Mario Mandzukic dakika ya 109 Croatia 2-1 England

Croatia ni taifa la watu milioni nne hivi na ni moja ya mataifa yenye idadi ndogo sana ya watu kuwahi kufika fainali Kombe la Dunia.

Watakutana na Ufaransa katika uwanja wa Luzhniki mjini Moscow Jumapili kwa fainali saa tatu usiku saa za Afrika Mashariki.

England watakutana na Ubelgiji mechi ya kuamua atakayemaliza nafasi ya tatu, mechi ambayo itachezewa mjini St Petersburg.

Kwa Croatia kukiwa kicheko na shangwe, kwa raia wa England kulienda masikitiko, huzuni na majonzi.

Haki miliki ya picha AFP/Getty Images
Image caption Mashabiki wakisherehekea Zagreb
Haki miliki ya picha AFP/Getty Images
Image caption Mashabiki wengi walijitokeza Zagreb
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mashabiki wakicheza kwenye maji kusherehekea katikati mwa mji wao mkuu Zagreb
Haki miliki ya picha AFP/Getty Images
Image caption Rais wa Croatia Kolinda Grabar-Kitarovic (kushoto) alimpa waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May jezi ya taifa hilo wakati wa mkutano mkuu wa Nato mjini Brussels, Ubelgiji
Haki miliki ya picha AFP/Getty Images
Image caption Kiongo wa kati wa Croatia Luka Modric (kati) akiwa na Mario Mandzukic (kulia) wakisherehekea Luzhiniki, Moscow
Image caption Shabiki huyu kwa jina Daniel alisherehekea kwa kinywaji, na aliambia BBC kwamba "ushindi huo ni mkubwa mno" kwa taifa hilo ndogo

Hali ilivyokuwa kwa England:

Walianza kwa matumaini baada ya bao kufungwa dakika za kwanza lakini baadaye wakavunjwa moyo.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ndoto kwisha: Mashabiki wakifarijiana katika bustani maarufu ya Hyde Park jijini London
Haki miliki ya picha PA
Image caption Shabiki mdogo wa England akiliwazwa Castlefield Bowl, Manchester

Katika bustani ya Hyde Park, London, takriban mashabiki 30,000 walifika kutazama England wakicheza nusufainali, mkusanyiko mkubwa wa watu London kutazama mchezo wa kandanda tangu Euro 96.

Haki miliki ya picha AFP
Image caption Shabiki huyu labda alizidi katika kusherehekea kabla ya mechi Urusi
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Shabiki wa England akisherehekea karibu na shabiki wa Croatia kabla ya mechi Urusi
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Maelfu ya mashabiki Hyde Park kabla ya mechi kumalizika
Haki miliki ya picha EPA
Image caption Wakati wa muda wa ziada Hyde Park
Haki miliki ya picha PA
Image caption Mashabiki wa England wakitokwa na machozi Manchester
Image caption Manchester wakisherehekea baada ya England kufunga bao la kwanza
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Mashabiki wakitokwa na machozi Brighton Beach
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mashabiki waliovalia barakoa za Harry Brighton Beach
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Shabiki wa England, Hyde Park
Haki miliki ya picha PA
Image caption Mashabiki walivyokuwa wakisherehekea awali Nottingham Castle
Image caption Lily Harkin mwenye miaka minane alikuwa ameandika mgongoni mwa Cole Bryceland, Nottingham kwa matumaini, 'Kombe linarejea nyumbani', lakini baadaye 'England walirejea nyumbani' bila kombe
Haki miliki ya picha Reuters
Image caption Roho mkononi Millennium Square, Leeds
Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Masikitiko Hyde Park