Kombe la Dunia 2018: Fifa yaonya vituo vya habari vinavyoangazia wanawake warembo uwanjani

Female football fans

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Federico Addiechi alisema shirikisho hilo la kandanda duniani linahitaji kusaidia kakabiliana na suala la kuibagua jinsia moja wakati wa Kombe la Dunia.

Vituo vya kutangaza mpira vimeamrishwa kutoelekeza kamera zao kwa wanawake warembo wanaokuwa miongoni wa mashabiki kwenye mechi zote za Kombe la Dunia, Fifa imesema.

Federico Addiechi alisema shirikisho hilo la kandanda duniani linahitaji kusaidia kakabiliana na suala la kuipendelea jinsia moja wakati wa Kombe la Dunia.

Kundi la kupinga ubaguzi la Fare Network linasema kuipendelea jinsia moja imekuwa tatizo kubwa kwenye kombe la dunia la Urusi mwaka 2018.

Fare Network inasema imekuwa ikifuatilia mechi na imekusanya zaidi ya visa 30.

Alipoulizwa ikiwa hatua hiyo itakuwa sera rasmi ya Fifa, Adiechi alisema ni moja ya masuala ambyo watakuwa nayo siku za usoni.

Kabla ya kombe la dunia kulikuwa na hofu kuwa ubaguzi wa rangi ingekuwa changamoto kuu, lakini mkurugenzi wa Fare Network Piara Powar alisema kupendelea jinsia moja ndilo lilikuwa lengo kuu kwa timu yake.

Powar pia aliongeza kuwa kuna visa kadhaa vya wanawawake maripota wakishikwa na kupigwa busu wakiwa bado hewani.

Alipoulizwa jinsi atakabiliana na hilo , Adiechi alisema wamekuwa wakishirikiana na wapangaji na polisi wa Urusi kuwatambua mashabiki hao.

Wakati wa mechi za Urusi mtandao wa picha wa Getty Images ulichapisha picha zilizoonyesha wanawake warembo wa Kombea la Dunia zilizoangazia wanawake wenye umri mdogo.

Picha hizo baadaye zilifutwa na Getty na ikasema kuwa imejutia makosa hayo.