Riyad Mahrez: Nataka nishinde ligi ya ubingwa na Mancity

Riyad Mahrez akifanya zoezi kwa mara yake ya kwanza akiwa Mancity

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Riyad Mahrez akifanya zoezi kwa mara yake ya kwanza akiwa Mancity

Nyota mpya wa Manchester City waliyemnasa kwa pauni milioni £60 kutoka Leicester, Riyad Mahrez sasa anadai lengo lake la kutua City ni kutwaa Champions League.

Mahrez, mwenye umri wa miaka 27, alijiunga na mabingwa hao wa ligi ya Premier kutoka Leicester Jumanne wiki hii.

Kiungo huyo wa Algeria, aliyetia wino mkataba wa maika 4, ameongeza kuwa amevutiwa na 'azma' ya klabu hiyo na fursa adhimu ya kunolewa na meneja mzoefu Pep Guardiola.

"City ina maazimio ya kuvuka hatua ya robo fainali Kombe la Champions League zaidi ya walivyofanya msimu uliopita," alisema.

"Nimefanya uamuzi wa kuwasili hapa kwa sababu nalenga kuhusika katika historia hiyo.

"Champions League ni ya mababe. City pia ni timu kubwa,wanakila kitu kujaribu na kulishinda. Pep ni meneta mtajika - ameshinda vitu vingi na kuweka historia klabu hii".

Maelezo ya sauti,

Cecafa itafaidi kutokana na urafiki mpya wa Eritrea na Ethiopia?

"Nitawekeza juhudi zangu zote kuiletea timu hii ufanisi. Na ikiwezekana niimarishe timu."

Lakini haitakuwa kazi rahisi kwa Mahrez, mshindi wa Premier League akiwa na Foxes wa Leicester 2016, kutokana na ushindani mkali wingi ya kushoto kutoka Leroy Sane, Bernardo Silva, Kevin de Bruyne na Raheem Sterling wanaocheza sehemu hiyo.

Hili sio tisho kwa Mahrez kwani amesema ushindani ni kawaida kwa kandanda na kwa timu zenye wachezaji wazuri hukumbwa na hali hiyo.

Dili hiyo ya usajili wa Mahrez,iliyokamilisha tetesi kati ya City na Leicester, ni ya sita kuwahi kuhusisha kiwango kikubwa cha pesa kutolewa na klabu ya Uingereza.