Tetesi za soka: Neymar, Jorghino, Unai Emery, Ivan Perisic na Antoinne Griezman

Neymar

Paris St-Germain imepiga jeki kukwama na mfungaji wa Brazil Neymar kwa kuimarisha mkataba wake na kuzima tamaa za Real Madrid dhidi ya kumshawishi 'mwanasarakasi' huyo mwenye umri wa maiak 26. (AS)

Meneja wa Arsenal Unai Emery ameweka wazi umuhimu wa kiungo wa Ujerumani Mesut Ozil kwa timu hiyo na kuongeza kuwa "umuhimu wake haumithiliki" katika klabu hiyo. Emery anamtaka Ozil arejee akiwa na fomu nzuri na baada ya kipindi hiki cha mapumziko kukamilika. (Guardian)

Klabu za ligi ya Premier zitapokea £30.75m kutoka Fifa inayofanya malipo ya pauni elfu £6,460-kila siku kumfidia kila mchezaji kila siku aliyeshiriki Kombe la Dunia. (Mirror)

Manchester United imeanza harakati za kufunga dili ya kumnyakua winga wa Inter Milan anayevuma sana Croatia Ivan Perisic, aliye na miaka 29. (Paris United, via Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images

Haifahimiki iwapo dili hii itashirikisha uhamisho wa beki wa Manchester United Matteo Darmian ambaye anakaribia kurejea Italia kuitumikia Inter Milan inayomhitaji raia huyo wa italia mwenye miaka 28 kwa njia ya mkopo. (Mirror)

Lakini Manchester United huenda isifanikiwe kumwahi beki wa Leicester na England Harry Maguire, 25, kwani klabu hiyo imeweka mkataba bora zaidi mezani ili kupandisha mapeni ya mlinzi huyo kutoka pauni elfu £45 hadi elfu £75 kumdumisha beki huyo klabuni. (Mail)

Nyota mwingine wa Leicester atakayetunukiwa mkataba mpya ni kiungo wa Nigeria Wilfred Ndidi ambaye ameihakikishia timu hiyo kusalia kwake baada ya kupinga madai kuwa aliwahi kuwaza juu ya kuihama klabu hiyo. (Leicester Mercury)

Chelsea imemtangaza meneja wa zamani wa Napoli Maurizio Sarri meneja wao mpya huku kocha huyo wa miaka 59 akisaini mkataba wa miaka miwili na uwezekano wa kuirefusha kwa miezi 12 zaidi. (Jarida la Times)

Huku Sarri akitabasamu, Kocha wa Chelsea aliyemtangulia, Antonio Conte ameachwa na manung'uniko huku akifunguka kuwa 'ameudhika' na jinsi blues walivyomng'oa kitini na sakata nzima ya kumpiga kalamu (Telegraph)

Wakati huo huo kiungo wa Napoli Jorginho, 26, naye amewasili pamoja na kocha wake wa zamani Sarri ugani Stamford Bridge huku wawili hao wakiwa ni mojawapo ya mageuzi ya soka Chelsea. (Guardian)

Mshambulizi wa Ufaransa Antoine Griezmann amemjibu kipa wa Ubelgiji anayecheza Chelsea Thibaut Courtois kwa kumrushia bonge la swali lililokejeli mpira wa Chelsea: "Kwani Thibaut Courtois anadhani hucheza mpira wa Barcelona kule Chelsea?". (Telegraph)

Haki miliki ya picha Getty Images

Sio wawili hao tu kwani Chelsea imeingia mzima mzima soko la uhamisho na kufikia sasa imekwisha fanya mazungumzo na Juventus kuhusu uhamisho wa mfungaji wa Argentina Gonzalo Higuain.Lakini Juventus inashikilia kuwa Higuain habanduki hadi nyota wa Blues Alvaro Morata, ajiunge na Juventus. (Mail)

Mtanunua nanyi mtanuna! Chelsea sio wa kununua lakini nao pia watalazimika kuwaachia baadhi ya mastaa wao kwani tayari klabu ya Uhispania ya Barcelona inamnyemelea kiungo mkabaji N'Golo Kante ofa yao ikiwa ni kumtoa Kiungo wa Ureno Andre Gomes, mwenye umri wa miaka 24 na pesa taslim ili kumhamisha kiungo wa Ufaransa Kante, mwenye miaka 27. (Sky Sports)

Huwezi kusikiliza tena
Cecafa itafaidi kutokana na urafiki mpya wa Eritrea na Ethiopia?
Haki miliki ya picha Getty Images

Tuondoka Chelsea tuingie Tottenham ambayo juhudi zake za kumkimbiza nyota wa Bordeaux Malcom, 21, zimegonga mwamba kwani staa huyo wa Brazil amefunga virago na anadaiwa kukaribia kufika Inter Milan kwa njia ya mkopo (Times)

Aidha, staa mwingine wa Brazil, anayepiga Lazio Felipe Anderson, mwenye miaka 25, anatarajiwa kukamilisha uhamisho hadi West Ham ya Uingereza siku chache zijazo baada ya kumaliza ukaguzi wa kimatibabu Ijumaa. (London Evening Standard)

Haki miliki ya picha Getty Images

Matumaini ya Newcastle kukamilisha biashara ya uhamisho wa winga wa Palace Andros Townsend, 26, inategemea uwezo wa Stoke kuishawishi Newcastle kumruhusu winga wake Matt Ritchie, 28 kuondoka klabu hiyo. (Newcastle Chronicle)

Kyle Bartley atatua West Brom baada ya Baggies kukubali milioni £4m kutoka Swansea. (Express and Star)

Tetesi kuwa Watford imekataa malipo ya zaidi ya pauni milioni £20m kutoka Everton kwa kiungo wa Ufaransa Abdoulaye Doucoure, 25, zimetajwa kuwa uongo mtupu! (Watford Observer)

Brighton inalenga kuimarisha safu yake na imeongeza kasi ya kunasa mkabaji wa Mali Yves Bissouma kutoka Lille, lakini Fulham pia inashukiwa kumtamani kiungo huyo mwenye miaka 21 (Argus)

Mada zinazohusiana