Tetesi za soka Ulaya Jumapili 15.07.2018: Mourinho, Pogba. Hazard na Courtois

Paul Pogba kwenda Barcelona?
Image caption Paul Pogba kwenda Barcelona?

Wakala wa Kiungo wa Manchester United Paul Pogba, 25, ameiambia klabu ya Barcelona ya Uhispania kuwa mchezaji huyo hana furaha na maisha yake ya soka chini ya Jose Mourinho. (Mundo Deportivo, via Mail on Sunday)

Real Madrid wako tayari kutoa kiasi cha pauni milioni 200 kumnasa Eden Hazard wa Chelsea, ambaye alidokeza kuwa anataka kuondoka Stamford Bridge. (Mail on Sunday)

Real pia wako kwenye hatua nzuri ya mazungumzo na mlinda mlango wa the Blues, Thibaut Courtois, (HLN, via Sunday Express)

Image caption Thibaut Courtois

Chelsea imetoa ofa ya mshambuliaji wa Uhispania Alvaro Morata, 25, kwa Juventus wakati ambapo nao wanajaribu kumsajili mshambuliaji wao, Gonzalo Higuain, 30. The Blues wanadhamiria kumuuza mshambuliaji wao Olivier Giroud miezi sita tu baada ya kumnunua kutoka Arsenal. (Sunday Mirror)

Mlinzi wa Manchester United na timu ya taifa ya England, Luke Shaw, 23, amekataa kusajiliwa Everton. (Sunday Times - subscription required)

Mshambuliaji wa Wales Gareth Bale, 28, atarejea Real Madrid kwa ajili ya mafunzo siku ya Jumatatu na anatarajiwa kufanya majadiliano na meneja mpya Julen Lopetegui kuhusu mustakabali wake . (Mail on Sunday)

Haki miliki ya picha PA
Image caption Luke Shaw

Napoli inaomba pauni milioni 80 kwa ajili ya mchezaji wa Senegal Kalidou Koulibaly likiwa ni jaribio la kuizuia Chelsea. (Sunday Mirror)

Arsenal inamtaka kiungo wa Juventus Rodrigo Bentancur, ambaye amewavutia alipokuwa akiwakilisha Uruguay kwenye michuano ya Kombe la Dunia. (Gazzetta dello Sport, via Daily Star Sunday)

Kiungo wa Tottenham na Ubelgiji Mousa Dembele, 30, amekataa kwenda Inter Milan lakini bado anataka kuondoka White Hart Lane majira haya ya joto. (Sun on Sunday)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp amesema mshambuliaji wa England Daniel Sturridge, 28,mustakabali wake unaweza kuwa Anfield. (Sky Sports)

Image caption Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp

Everton na Bournemouth wanafikiria kumchukua kiungo wa Genoa na Uruguay Diego Laxalt.(Sun on Sunday)

Cardif City wanamtolea macho winga Matt Phillips, 27, wa West Brom na Scotland sambamba na Middlesbrough na Newcastle. (Mail on Sunday)

Beki wa kushoto wa Manchester United Demetri Mitchell, 21 anatakiwa na Derby County. (Sun on Sunday)

United ni miongoni mwa klabu kadhaa zinazotaka kumsajili kiungo kutoka timu ya taifa vijana ya England wa chini ya miaka 17Dylan Crowe, ambaye amepewa ofa ya kukipiga Ipswich.(Goal)

Bora kutoka Jumamosi

Paris St-Germain imepiga jeki kukwama na mfungaji wa Brazil Neymar kwa kuimarisha mkataba wake na kuzima tamaa za Real Madrid dhidi ya kumshawishi 'mwanasarakasi' huyo mwenye umri wa maiak 26. (AS)

Meneja wa Arsenal Unai Emery ameweka wazi umuhimu wa kiungo wa Ujerumani Mesut Ozil kwa timu hiyo na kuongeza kuwa "umuhimu wake haumithiliki" katika klabu hiyo. Emery anamtaka Ozil arejee akiwa na fomu nzuri na baada ya kipindi hiki cha mapumziko kukamilika. (Guardian)

Klabu za ligi ya Premier zitapokea £30.75m kutoka Fifa inayofanya malipo ya pauni elfu £6,460-kila siku kumfidia kila mchezaji kila siku aliyeshiriki Kombe la Dunia. (Mirror)

Manchester United imeanza harakati za kufunga dili ya kumnyakua winga wa Inter Milan anayevuma sana Croatia Ivan Perisic, aliye na miaka 29. (Paris United, kupitia Sun)

Nyota mwingine wa Leicester atakayetunukiwa mkataba mpya ni kiungo wa Nigeria Wilfred Ndidi ambaye ameihakikishia timu hiyo kusalia kwake baada ya kupinga madai kuwa aliwahi kuwaza juu ya kuihama klabu hiyo. (Leicester Mercury)

Wakati huo huo kiungo wa Napoli Jorginho, 26, naye amewasili pamoja na kocha wake wa zamani Sarri ugani Stamford Bridge huku wawili hao wakiwa ni mojawapo ya mageuzi ya soka Chelsea. (Guardian)

Mshambulizi wa Ufaransa Antoine Griezmann amemjibu kipa wa Ubelgiji anayecheza Chelsea Thibaut Courtois kwa kumrushia bonge la swali lililokejeli mpira wa Chelsea: "Kwani Thibaut Courtois anadhani hucheza mpira wa Barcelona kule Chelsea?". (Telegraph)

Mada zinazohusiana