Tetesi za soka Ulaya Jumatatu 16.07.2018: Milinkovic-Savic,Courtois, Luke Shaw

Sergej Milinkovic-Savic Haki miliki ya picha AFP
Image caption Sergej Milinkovic-Savic

Chelsea ina hamu kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Lazio, Sergej Milinkovic-Savic msimu huu wa joto. Mchezaji huyu mwenye umri wa miaka 23 amehusishwa na uhamisho kwenda Manchester United. (Corriere dello Sport, via Talksport)

Kipa wa Chelsea raia wa Ubelgiji Thibaut Courtois anasema mkataba aliopewa na the Blues ni "tofuati kuliko mwingine ninaoweza kupata" kwingine. Mchezjai huyo amehusishwana uhamisho kwenda Real Madrid. (Mirror)

Courtois anasema mchezaji mwenzake wa Chelsea Eden Hazard: "Ninako kwenda, Hazard lazima anifuate." Hazard, wa miaka 27, pia amehusishwa na uhamisho kwenda Real Madrid. (Evening Standard)

Liverpool imewasilisha ombi kutaka kumsajili kipa wa Barelona raia wa Uholanzi Jasper Cillessen, mwenye miaka 29. (Mundo Deportivo, via Talksport)

Didier Deschamps asema ushindi wa Ufaransa ni miujiza.

Mchezo wa kandanda asili yake ni wapi?

Mlinzi wa England Luke Shaw, wa miaka 23, yupo tayari kuondoka Manchester United kama ajenti wa bure iwapo hatothibitishwa kuwa chaguo la kwanza la Jose Mourinhokiungo cha beki kushoto msimu huu. (Manchester Evening News)

Haki miliki ya picha PA
Image caption Luke Shaw alikuwa mojawapo ya vijana wanaolipwa fedha nyingi alipojiunga na Manchester United kwa pauni milioni 27 kutoka Southampton 2014

Everton, Tottenham na Chelsea zote zinamtaka mchezaji wa kiungo cha kati wa Boca Juniors Wilmar Barrios, wa miaka 24. (TyC Sport, via HITC)

Mwenyekiti wa Lyon chairman Jean-Michel Aulas anakaribisha kuanzishwa upya jitihada za Liverpool kumsajili mshambuliaji wa Ufaransa Nabil Fekir, wa miaka 24. (Le10 Sport, via Liverpool Echo)

Besiktas wamepewa mshambuliaji wa West Ham Andy Carroll, wa miaka 29, kwa mkopo. (Fanatik, via 90min)

Meneja wa Derby Frank Lampard anakaribia kumsaini winga wa Liverpool Harry Wilson, kwa mkopo. (Mirror)

Ufaransa washinda Kombe la Dunia kwa kuwachapa Croatia 4-2

Everton wana hamu ya kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Espanyol David Lopez. Mchezaji huyo wa miaka 28 pia analengwa na Valencia na Real Betis. (Mundo Deportivo)

Haki miliki ya picha Getty Images

​​Brighton wapo tayari kuwapiku Porto katika kumsajili mchezaji wa kiungo cha kati wa Mali Yves Bissouma, mwenye umri wa miaka 21, kutoka klabu ya Lille katika Ligue 1. (Record, via 90min)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Manchester raia wa Uhispani Brahim Diaz, wa miaka 18, anasema hataki kuchukuliwa kw amkopo msimu ujao ili kupata fursa ya kucheza katika timu ya kwanza. (Manchester Evening News)

Rais wa Napoli Aurelio de Laurentiis anasema timu hiyo ya Serie A walipendekezewa Cristiano Ronaldo kabla ya mreno huyo mwenye umri wa miaka 33 kujiunga na Juventus kutoka Real Madrid. De Laurentiis aliamua kutomsajili Ronaldo kwasababu 'ingehatarisha klabu hiyo kufilisika'.(Gazzetta dello Sport, via Goal)

Leicester City wamemsaini msambuliajiw a zamani wa Tottenham Ryan Loft, mwenye umri wa miaka 20, katika mkataba wa miaka miwili. (Sky Sports, via Leicester Mercury)

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii