Ghasia zazuka Paris sherehe za kushinda Kombe la Dunia
Huwezi kusikiliza tena

Ghasia zazuka Paris, Ufaransa sherehe za kushinda Kombe la Dunia

Ufaransa wanasherehekea kushinda Kombe la Dunia kwa mara ya pili katika kipindi cha miaka 20.

Hata hivyo, sherehe hizo katikati mwa Paris ziligeuka karaha baada ya mashabiki kuzua fujo na kukabiliana na maafisa wa usalama.

Ghasia zilishuhudiwa zaidi karibu na barabara ya Champs Elysees.