Pussy Riot: Waliovamia uwanja wakati wa fainali ya Kombe la Dunia Urusi washtakiwa

A pitch invader high fives France's Kylian Mbappé during the 2018 FIFA World Cup final football match between France and Croatia, 15 July 2018
Maelezo ya picha,

Mmoja wao alimfikia Kylian Mbappé kabla ya uondolewa kwa nguvu uwanjani

Maafisa nchini Urusi wamewafunguliwa mashtaka wanachama wanne wa kundi la Pussy Riot kwa kuvuruga mechi ya fainali walipoingia uwanjani mechi ya fainali ikiendelea.

Wameshutumiwa kwa kukiuka sheria zilizowekwa kwa mashabiki katika mashindano pamoja na kuvaa sare za polisi kinyume na sheria.

Makosa hayo yanavutia faini ya kati ya pauni (£121 na $161) yaani pesa za Urusi roubles 10,000 na 1,500, mtawalia.

Pussy Riot imejitetea kuwa maandamano yao yalikuwa yanapinga ukiukaji wa haki za kibinadam Urusi.

Walinzi wa usalama waliwachuja kutoka uwanjani.

Tukio hilo lilikatiza kipindi cha pili mechi ya fainali kati ya Ufaransa na Croatia na kusitisha mechi kwa takriban sekunde 25.

Ufaransa ilijinyakulia ushindi wa 4-2.

Usalama ulikuwa ni wa hali ya juu na haifahamiki jinsi wanaharakati hao walivyoingia uwanjani namna gani.

Pussy Riot wamewahi kuandaa maandamano ya hali ya juu dhidi ya rais Vladimir Putin hapo awali.

Maelezo ya picha,

Wanachama hao walifanikiwa licha ya ulinzi mkali uliokuwepo

Wanachama wake watatu walikamatwa mnamo 2012 kwa kutunga wimbo dhidi ya Rais Putin ulioandaliwa jengo la kanisa kuu la Moscow.

Kundi hilo limeeleza kuwa wanachama wake waliokamatwa Jumapili walimaliza usiku kucha ndani ya kituo cha polisi katika hali mbaya na watafikihswa mahakamani kuhukumiwa kwa "makosa ya usimamizi".

Hisia mseto

Wanawake watatu na mwanamume mmoja walikimbia kuingia uwanjani,ingawa mmoja wao alipigwa rafu na kutofanikiwa kuingia. Walivaa sare zilizofanana na za maafisa wa polisi: Shati nyeupe, suruali nyeusi na madaraka.

Mwanaharakati mmoja wa kike alifanikiwa kupokezana salamu na nyota wa Ufaransa Kylian Mbappé kabla ya kuondolewa uwanjani.

Ingawa wanawake wote watatu walitua hadi kitovu cha uwanja, mwenzao wa kiume alinaswa kwa ghadhabu na beki wa Croatia Dejan Lovren.

Maelezo ya picha,

Lovren alimkamata mmoja wao

Baada ya hapo, Lovren aliwaambia waandishi: "Nilizidiwa na hisia na kumkaba jamaa huyo na natamani ningekuwa na uwezo wa kumrusha hadi nje ya uwanja."

Beki Lovren alimkamata, mmoja wa waharibifu hao.

Mtu huyo alitajwa kuwa Pyotr Verzilov, mumewe Nadezhda Tolokonnikova, mmoja wa wanaharakati watatu wa kundi hilo la Pussy Riot waliokamatwa 2012.

Wanawake hao wametambuliwa kuwa Nika Nikulshina, Olga Kurachyova na Olga Pakhtusova.

Kulingana na taarifa kutoka kwa kundi hilo Pussy Riot, wamejitetea kuwa lengo la tendo lao lilikuwa ni la kutoa ujumbe kwa mamlaka za Urusi:

  • Kuwaachilia wafungwa wa kisiasa
  • Kupinga kuwakakamata raia katika mikutano ya hadhira.
  • Kuruhusu ushindani wa kisiasa nchini humo.
  • Kuzuia kubuni kesi zisizokuwa na ukweli na kuwazuia watu gerezani bila sababu.

Mtetezi na mwanablogu anayempinga Putin Alexei Navalny ameachia ujumbe wa video kwenye ukionyesha mmoja wa waandamanji walioingia uwanjani akiulizwa maswali ya kuchunguzi na maafisa wa polisi.

Jamaa mmoja anaskika akizungumza kwa hasira na bwana Verzilov huku naye mwanawake aliyekamatwa akionekana akiwa katika hali mbaya akiwa amevaa sare zake za polisi.

"Mara nyingine natamani tungekuwa 1937" mtu mmoja anaskika nje ya kamera, kama njia ya kukubaliana na kipindi cha kuogofya na ukatili chini ya uongozi wa kiimla wa dikteta wa Kisovieti Joseph Stalin.