Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 17.07.2018

Gareth Bale
Maelezo ya picha,

Gareth Bale

Manchester United huenda wakakosa kumsaini Gareth Bale wakati mshambuliaji huyo kutoka Wales mwenye miaka 29 anatarajiwa kuambiwa kuwa yuko kwenye mipango ya meneja mpya wa Real Madrid Julen Lopetegui. (Metro)

Manchester City hawataki kutimiza ofa ya Real Madrid ya pauni milioni 80 kwa kiungo wa kati raia wa Croatia mwenye umri wa miaka 24 Mateo Kovacic. (Sky Sports)

Maelezo ya picha,

Gonzalo Higuain

Chelsea wanazungumzia mipango ya kumnunua mshambuliaji wa Juventus raia wa Argetina Gonzalo Higuain, 30 kwa pauni milioni 53. (Evening Standard)

Newcastle na Celtic wanammezea mate kiungo wa kati wa Uruguay Giorgian de Arrascaeta, 24, ambaye thamani yake imewekwa kuwa milioni 18 na Cruzeiro. (Sun)

Monaco wametangaza ofa kwa CSKA Moscow kwa kiungo wa kati mrusi mwenye miaka 22 Aleksandr Golovin, ambaye pia amehusishwa na ofa ya pauni milioni 22 ya kuhamia Chelesea. (Sport Express - in Russian)

Maelezo ya picha,

Danny Ings

Southampton wamejitenga kutokana na ripoti kuwa wanamwinda mchezaji wa Liverpool mwenye miaka 25 raia wa England Danny Ings. (Daily Echo)

Meneja wa Arsenal Unai Emery anapanga kukipunguza kikosi chake na hatma ya mshambuliaji wa Engaland Danny Welbeck, 27, na kipa raia wa Colombia David Ospina, 29, hazijulikani. (Telegraph)

Maelezo ya picha,

Wilfried Zaha

Wing'a wa Crystal Palace Wilfried Zaha haendi popote kwa miaka minne kulingana na meneja Roy Hodgson. Mchezaji huyo wa kimataiafa raia wa Ivory Coast analengwa na Everton, Tottenham na Borussia Dortmund. (Liverpool Echo)

Mshambuliaji wa Leicester raia wa Nigeria Ahmed Musa, 25, anahusishwa sana na mpango wa pauni milioni 40 wa kuhamia klabu ya Saudi Arabia. (Leicester Mercury)

Maelezo ya picha,

Mousa Dembele

Fernerbahce wamemfanya mshambulizi wa Tottenham mbelgiji Mousa Dembele, 31, lengo lake wakati wanataka kuboresha zaidi kikosi chao. (Fanatik, via 90min)

Mlinnzi wa Newcastle raia wa England Jamaal Lascelles, 24, hana nia ya kuondoka licha ya kumezewa mate na vilabu vya ligi ya Primia. (Times - subscription required)

Maelezo ya picha,

Nabil Fekir

Kiungo wa kati wa Lyon raia wa Ufaransa Nabil Fekir, 24, amesema kuwa kuna uwezekano uenda ahamie Liverpool . (Metro)

Rais wa Real Sociedad Jokin Aperribay amekana kumwindwa beki wa Arsenal Nacho Monreal, 32. (Mundo Deportivo, via Football London)

Derby wanakaribia kumsaini kiungo wa kati wa England youth Mason Mount, 19, kwa mkopo kutoka Chelsea. (Telegraph)

Maelezo ya picha,

Jose Fonte

Nahodha wa Southampton Jose Fonte, 34 hana klabu wakati mkataba wa mlinzi huyo raia wa Ureno kwenye klabu Dalian Yifang ya China kufutwa mapema. (Daily Echo)

Atletico Madrid karibu wanakamilisha kumsaini mshambuliaji wa AC Milan na Croatia Nikola Kalinic, 30. (Marca - via Football Italia)

Maelezo ya picha,

Nikola Kalinic

Bingwa wa olimpiki Usain Bolt 31, yuko karibu kusaini mkataka wa kujiunga na klabu ya Ligi A Central Coast Mariners. (Telegraph)

Fulham wametoa ofa ya pauni milioni 1.3 kwa kipa wa Espanyol Roberto Jimenez, 32. (Lacontra Deportivo - in Spanish)

Chelsea wamefikia makubaliano ya kumuuza kiungo wa kati raia wa Ivory Coast Jeremie Boga, 21, kwenda klabu ya Sassuolo ya Italia kwa pauni milioni 3.5. (Goal)