Cristiano Ronaldo: Wachezaji wa umri wangu huelekea Qatar au China

Cristiano Ronaldo
Maelezo ya picha,

Ronaldo akipokelewa huko Allianz mjini Turin jana jumatatu

Cristiano Ronaldo anasema anashukuru kwa fursa aliyopewa na Juventus kwa kuwa wachezaji wa umri wake mara nyingi huelekea Qatar au China.

Mchezaji huyo wa miaka 33 mshambuliaji raia wa Ureno alijiunga na mabingwa hao wa Italia kwa pauni milioni 99.2 baada ya miaka 9 huko Real Madrid.

"Kujiunga na klabu hii wakati huu wa taaluma yangu, nina furaha sana," alisema wakati akikaribishwa kwenye klabu hiyo huko Turin.

Ronaldo pia alisema ana matumaini kuwa atakuwa nyota mwenye bahati wakati klabu hiyo ya Italia inajaribu kushinda ubingwa wa ligi.

Aliongeza kuwa hajapata ofa kutoka kwa klabu yoyote.

Ronaldo aliweka rekodi ya magoli 450 akiwa na Real Madrid, akashinda ubingwa mara nne na La liga, mara mbili baada ya kujiunga na Manchester City mwaka 2009.

Maelezo ya picha,

Ronaldo alipokelewa huko Allianz mjini Turin jana jumatatu

Mshindi huyo mara tano wa tuzo la Ballon d'Or - ukiwemo wa mwaka uliopita - aliiongoza Ureno kupata ushindi wa Ulaya mwaka 2016.

"Ninataka kushinda, ninataka kuwa bora zaidi. Labda ninaweza kupewa tuzo la Ballon d'Or tena."

"Ilikuwa vigumu kulishinda huko Manchester na Real Madrid, lakini labda hapa? Tutaona."

Juventus ndiyo klabu bora zaidi nchini Italia baada ya kushinda ligi ya Serie A mara 34 zikiwemo saba zilizopita mfululizo na Coppa Italia mara 13.

Hata hivyo hawajashinda ligi ya mabingwa tangu mwaka 1996 wakiwa wanapoteza katika fainali mara tano.

Maelezo ya picha,

Cristiano Ronaldo akisalimia mashabiki wa Juventus uwanja wa Allianz