Tetesi za Soka Ulaya Jumatano 18.07.2018

Eden Hazard
Maelezo ya picha,

Eden Hazard

Real Madrid wamemweka mshambuliaji wa Chelsea na Ubelgiji Eden Hazard, 27 nambari moja kwenye orodha ya wachezaji inaowawinda kuchukua mahala pake Cristiano Ronaldo, ambaye amejiunga na Juventus. (Star)

Kipa wa Chelsea na Ubelgiji Thibaut Courtois, 26, anatarajiwa kujiunga na Real Madrid kwa payuni milioni 31. (Marca - in Spanish)

Maelezo ya picha,

Petr Cech

Ikiwa watamuuza Courtois, Chelsea watatathmini kumsaini kipa wa miaka 36 raia wa Czech Petr Cech kutoka Arsenal au kutoka Leicester raia wa Denmark Kasper Schmeichel, 31. (Sky Sports)

Nahodha wa Chelsea Gary Cahill, 32, anatathmini kukamilisha taaluma yake ya miaka sita huko Stamford Bridge mwisho mwa mwezi huu wakati klabu hiyo inafikia makubaliano ya paunia milioni 44.2 kwa mlinzi wa Jeventus na Italia Daniele Rugani. (London Evening Standard)

Chelsea bado wako mbioni kumsaini kipa wa Roma raia wa Brazil Alisson licha ya Liverpool kutoa ofa ya pauni milioni 62 kwa mchezaji huyo mwenye miaka 25. (Football Italia)

Maelezo ya picha,

Zinedine Zidane

Aliyekuwa meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane, 46, atajiunga na Juventus, klabu ambayo raia huyo wa Ufaransa aliichezea kati ya mwaka 1996 na 2001 kama mshauri. (Libertad Digital)

Everton wako kwenye mazungumzo kumsaini wing'a wa Bordeauxraia na Brazil Malcolm, 21, kwa pauni milioni 30m. (Sky Sports)

Maelezo ya picha,

Jefferson Lerma

Bournemouth watatumia pesa nyingi zaidi katika historia ya klabu ambazo ni pauni milioni 31 kumsaini kiungo wa kati wa Levante na Colombia Jefferson Lerma, 23, na zingine pauni milioni 25 kwa beki wa Genoa na Uruguay Diego Laxalt, 25. (Sun)

Meneja wa Newcastle raia wa Uhispania Rafael Benitez, 58, hana furaha baada ya kuambiwa kuwa ni lazima auze kablay a kuboresha kikosi chake. (Mirror)

Maelezo ya picha,

Chancel Mbemba

Porto bado wanataka kumsaini mlinzi wa Newcastle Chancel Mbemba, 23, lakini hawataki kutimiza bei aliyowekewa ya pauni milioni 8 kwa mchezaji huyo wa kimataifa raia wa Congo. (A Bola - in Portuguese)

West Brom wamekataa ofa ya mkopo kwa mashambuliaji wa Newcastle raia wa Venezuela Salomon Rondon, 28, ambaye mkataba wake una kipengee cha kuondoka cha milioni 16.5. (Express and Star)