Alex Oxlade-Chamberlain: Kiungo wa kati wa Liverpool kukosa kipindi kirefu cha 2018-19

Alex Oxlade-Chamberlain

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Alex Oxlade-Chamberlain aliichezea Liverpool msimu uliopita na kufunga magoli matano

Kiungo wa kati wa Liverpool na Uingereza Alex Oxlade-Chamberlain anatarajiwa kukosa kipindi kirefu cha msimu wa 2018-19 kulingana na mkufunzi Jurgen Klopp.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 hajacheza tangu alipopata jereha la goti wakati wa mechi ya nusu fainali ya kombe la vilabu bingwa Ulaya dhidi ya Roma mnamo mwezi Aprili.

Tunahisi sasa ndio wakati mwafaka kuwaambia watu kwamba Ox , msimu huu utakuwa wa kuuguza jeraha, alisema Klopp.

Tulijua hili tangu alipopata jeraha hilo. OX-laide Chamberlain alikosa kombe la dunia baada ya kupata jeraha la goti wakati alipokuwa akimkabili mchezaji wa Roma Aleksandar Kolarov katika uwanja wa Anfield tarehe 24 April.

Akicheza mara 32 , alihamia Liverpool kutoka Arsenal msimu uliopita kwa dau la £35m.

Oxlade-Chamberlain alifanyiwa upasuaji msimu uliopita, lakini Klopp alisema kuwa mchezaji huyo hakutaka ubaya wa jeraha hilo kutajwa wakati huo kwa kuwa ungeathiri kampeni ya kutaka kushinda kombe la vilabu bingwa.

Liverpool ilishindwa 3-1 katika fainali na Real Madrid.

Chanzo cha picha, Alexoxchamberlain

Maelezo ya picha,

Alex Oxlade-Chamberlainalichapisha picha hii katika mtandao wake wa Instagram

"Hakuna mabadiliko yoyote , kila kitu kimekwenda kulingana na wakati tulioweka'', alisema Klopp. Habari mpya ni kwamba sasa tumeanza kutoa habari kuhusu jeraha hilo hadharani.

''Hatukutaka habari hizi kuathiri mwisho wa msimu, kwa kweli tuliona ni vyema kuzungumza wakati unaofaa''.