Liverpool: Kipa Alisson atua Liverpool tayari kuchukua mahala pake Karius

Alisson

Chanzo cha picha, Getty Images

Uuzaji wa kipa Alisson kuelekea Liverpool hauonyeshi ukosefu wa tamaa , kulingana na mkurugenzi wa kandanda katika klabu ya Roma Monchi ambaye amekiri kwamba uhamisho wa mchezaji huyo wa Brazil ulikuwa mgumu kwa mashabiki kuelewa.

Liverpool imeamua kumnunua kipa huyo kwa dau la £66.8m .

Roma inasema kuwa Alisson tayari amewasili katika klabu hiyo ya Anfield huku mazungumzo yakidaiwa kupiga hatua kubwa. Wakati ombi zuri linapokuja ni vyema kulitafakari, alisema Monchi .

Tulipima uzitoi wake na kuamua kuzungumza na Liverpool.Uuzaji wa Alison hauonyesha kwamba hatuna tamaa .

Kwangu mimi tamaa ni kufanyauamuazi wa sawa baada ya kupima kila kitu. Ombi la Liverpool ambalo ni Yuro 70m litaipiku rekodi ya uhamisho wa kipa ya Yuro 53m zilizolipwa na Juventus kwa Parma kumnunua kipa Gianluigi Buffon 2001.

Chanzo cha picha, Getty Images

Alisson mwenye umri wa miaka 25, amekuwa katika klabu ya Roma kwa miaka miwili na alishirikia katika mechi 37 za ligi ya Seria A baada ya kuanza soka ya kulipa katika klabu ya Brazil ya Internacional.

Mkufunzi wa Liverpool Jurgen Klopp alilazimishwa kumtetea kipa wa klabu hiyo Loris Karius wiki iliopita baada ya kufanya makoa mengine-wakati huu katika mechi ya kiurafiki ya kujiandaa kwa msimu mpya dhidi ya Tranmere.

Kipa huyo wa Ujerumani mwenye umri wa miaka 25 aliutema mpira wa mkwaju wa adhabu ambao uliwasaidia wapinzani kufunga katika mechi ambayo Liverpool iliibuka washindi kwa 3-2 katika uwanja wa Prenton Park.

Karius alifanya makosa mawili ambayo yaliigharimu Liverpool katika mechi ya fainali ya vilabu bingwa Ulaya ambapo ilishindwa 3-1 na Real madrid- kabla ya kubainika baadaye kwamba alikuwa na mshtuko.

Alisson alicheza mechi zote tano, na kutufungwa tatu , huku Brazil ikiondolewa katika katika awamu ya robo fainali katika kombe la dunia na Ubelgiji.