Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 22.07.2018

Eden Hazard Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Eden Hazard

Chelsea wamewaambia Real Madrid kuwa hawawezi kulazimishwa kumuuza kiungo wa kati raia wa Ubelgiji mwenye miaka 27 Eden Hazard - hata kwa kima cha pauni milioni 170. (Mirror)

Rais wa Napoli Aurelio de Laurentiis ameonya kuwa meneja wake wa zamani Maurizio Sarri, ambaye sasa anaisimamia Chelsea kuwa hakutakuwa tena na makubaliano kati ya vilabu hivyo viwili. (Goal)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Marcos Rojo

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho bado anamfikiria mlinzi wa Leicester Harry Magun na atatoa ofa ya pauni milioni 65 kwa raia huyo wa England mwenye miaka 25 lakini kwanza atahitaji kumuachia Marcos Rojo, Eric Bailly au Chris Smalling. (Mail)

United wako tayari kumuongezea mkataba Anthony Martial ambao utamwezesha mshambuliaji huyo mfaransa mwenye miaka 22 kubaki nao hadi mwaka 2020. (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Andreas Pereira

Chelsea na Bayern Munich wanataka kumsaini Martial, licha ya kutokuwepo na klabu kati yao kinachotaka kitimiza ofa ya United ya pauni milioni 89.9 aliyewekewa mchezaji huyo. (Times)

Kiungo wa kati raia wa Brazil Andreas Pereira, 22, amemuambia meneja wa Manchester United Mourinho kuwa yuko tayari kucheza wakati wowote anapohitajika (Manchester Evening News)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Yann Sommer

Arsenal wamepiga hatua kawenye amzunguzmoa ya kumsainia kipa wa Borussia Monchengladbach raia wa Uswizi. Yann Sommer, 29. (Express)

Aliyekuwa mlinzi wa Chelsea na Aston Villa John Terry, 37, anaripotiwa kustaafu kutoka kandanda huku kituo cha Sky Sports kikitaka ajiunge nacho. (Mirror)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Petr Cech

Roma wanataka kumsaini kipa wa Arsenal Petr Cech, 36 kuchukua mahala pake kipa aliyehamia Liverpool Alisson. (Sun)

Atletico Madrid wamezungumza na Chelsea kuhusu uwezekano wa kumsaini mshambuliaji wa Ufaransa Olivier Giroud, 31, kwa mkopo. (Sky Sports)

Meneja wa Newcastle, Rafa Benitez atapewa kitita cha pauni milioni 100 kununua wachezaji ikiwa atakubali mkataba mpya wa miaka mitatu. (Sun)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Rafa Benitez

Leicester watakubali ofa ya karibu pauni milioni 18 kumsaini Islam Slimani. Mashambuliaji huyo wa miaka 30 raia wa Algeria amehusishwa na kuhamia Sporting Lisbon. (Leicester Mercury)

Leicester wamekataa ofa ya pauni milioni 12 kutoka klabu ya Saudi Arabia Al Nassr kwa mshambuliaji raia wa Nigeria Ahmed Musa, 25. (Mail)