Mesut Ozil atetea picha yake na rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan

lkay Gundogan and Mesut Ozil, along with Everton's Cenk Tosun, pose with the Turkish president Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ilkay Gundogan na Mesut Ozil pamoja na Cenk Tosun wa Everton wakiwa na rais wa Uturuki

Kiungo wa kati wa Arsenal Mesut Ozil amesema angewakosea heshima mababu zake iwapo angekataa kupigwa picha pamoja na rais wa Uturuki.

Ozil na mchezaji wa Manchester City Ilkay Gundogan, wachezaji wa Ujerumani walio na asili ya Uturuki walikosolewa na shirikisho la kandanda nchini Ujerumani kwa kukutana na Recep Tayyip Erdogan mwezi Mei

Katika taarifa Ozil alisema "haikuhusu siasa au uchaguzi".

"Nina miyo wili mmoja wa kijerumani na mwingine wa kituruki, alisema kupitia Twitter.

Ni kuhusu mimi kuwakilisha ofisi ya juu zaidi ya nchi ya familia yangu".

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mesut Ozil akimkabihdi Recep Tayyip Erdogan shati

"Wakati nikiwa mtoto, mama yangu alinifunza kuwa kila wakati niwe na heshima na kamwe nisisahau nilikotoka."

Baada ya wachezaji hao kukutana na Erdogan kwenye warsha moja mjini London, ambapo Ozil anasema walizungumzia kuhusu kandanda, picha zilitolewa na chama tawala nchini Uturuki wakati wa kukaribia uchaguzi wa nchi hiyo ambao ulishindwa na Erdogan.

Wanasiasa wengine nchini Ujerumani waliwakosoa Ozil na Gundogan na kutilia shaka uzalendo wao kwa Ujerumani.

Ujerumani awali ilikuwa imemkosoa rais huyo wa Uturuki kutokana na kampeni yake dhidi ya wapinzani kufuatia mapinduzi yaliyofeli.

Mada zinazohusiana