Mesut Ozil: Shirikisho la soka Ujerumani lakataa madai ya ubaguzi ya mshambuliaji wa Arsenal

Mesut Ozil Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ozil hakuweza kuzuia Ujerumani isifungwe na Korea kusini katika Kombe la Dunia awamu ya makundi

Shirikisho la soka Ujerumani 'limekataa pasi na shaka 'tuhuma za ubaguzi wa rangi kutoka kwa mshambuliaji wa Arsenal Mesut Ozil lakini linasema huenda lingewajibika zaidi katika kuhakikisha mchezaji huyo hakunyanyaswa.

Ozil, mwenye umri wa miaka 29, alitangaza kujiuzulu katika soka ya kimataifa, akitaja "ubaguzi wa rangi na ukosefu wa heshima" ndani ya soka Ujerumani.

Mchezaji huyo wa kiungo cha kati amesema amepokea barua za chuki na vitisho na alilaumiwa kwa kushindwa Ujerumani katika Kombe la Dunia.

Shirikisho hilo la soka DFB limeeleza kuwa 'limesikitishwa na kuondoka kwa

Limeongeza katika taarifa yake: "Tunakataa pasi na shaka kuhusishwa DFB na ubaguzi wa rangi. DFB limejishughulisha na suala la utengamano Ujerumani kwa miaka mingi."

Ozil alishutumiwa na DFB na katika vyombo vya habari Ujerumani baada ya kupigwa picha na rais wa Uturuki anayekumbwa na mzozo Recep Tayyip Erdogan katika hafla moja London mnamo Mei.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Ilkay Gundogan na Mesut Ozil pamoja na Cenk Tosun wa Everton wakiwa na rais wa Uturuki

Alishutumiwa zaidi baada ya Ujeurmani kutolewa katika awamu ya makundi kwenye Kombe la Dunia.

Mesut Ozil atetea picha yake na rais wa Uturuki

DFB limekiri kwamba huenda halikulishughulikia suala hilo ipasavyo, likiongeza: " Inasikitisha kuwa Mesut Ozil amehisi hakulindwa vya kutosha dhidi ya kauli za kibaguzi."

Je yote haya yalianza vipi?

Ozil, ambaye kwa kizazi cha tatu ni Mjerumani mwenye asili ya Uturuki, alizaliwa huko Gelsenkirchen na alichangia pakuu ushindi wa nchi yake katika mashindano ya 2014 Kombe la Dunia.

Mweiz mmoja kabla ya Ujerumani kutetea taji lake, Ozil alikutana na rais wa Uturuki Erdogan pamoja na wachezaji wenza wa Ujerumani Ilkay Gundogan, mchezaji wa Manchester City ambaye pia ana asili ya Uturuki.

Baada ya hapo picha zilisambazwa na chama tawala cha Uturuki AK Party kuelekea uchaguzi katika nchi hiyo ambapo Erdogan aliibuka mshindi mwezi uliopita.

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Mesut Ozil ajishikilia kichwa baada ya Ujerumani kutolewa katika Kombe la Dunia

Wanasiasa wengine nchini Ujerumani waliwakosoa Ozil na Gundogan na kutilia shaka uzalendo wao kwa Ujerumani.

Ujerumani awali ilikuwa imemkosoa rais huyo wa Uturuki kutokana na kampeni yake dhidi ya wapinzani kufuatia mapinduzi yaliyofeli.

Wachezaji hao walikutana na rais wa shirikisho la soka Ujerumani kueleze kilichotukia, licha ya kwamba Ozil hakutoa tamko hilo hadharani kuhusu suala hilo hadi Jumapili.

Alisema Erdogan alikutana na Malkia wa Uingereza na waziri mkuu Theresa May akiwa England na akaeleza kwamba angekuwa amewakosea heshima mababu zake iwapo angekataa kupigwa picha pamoja na rais wa Uturuki.

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii