Man City 1-2 Liverpool: Mohamed Salah na Sadio Mane waifungia timu yao

Sadio Mane afunga mkwaju wa penalti dhidi ya Manchester City

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola aliwapongeza wachezaji wake kwa juhudi zao baada ya kushindwa na Liverpool kufuaia penalti iliofungwa na Sadio Mane

Mohamed Salah hakupoteza wakati wowote katika ufungaji wa mabao baada ya Liverpool kutoka nyuma na kuishinda Manchester City 2-1 mjini New Jersy Marekani.

Mshambuliaji huyo wa Misri , ambaye alifunga mabao 44 katika mechi 52 msimu uliopita alisawazisha bao lililofungwa na Leroy Sane katika kipindi cha pili dakika moja baada ya kuingia kama nguvu mpya mbele ya umati wa mashabiki 52,000.

Kichwa chengine cha Salah kilipanguliwa na kugonga chuma cha goli.

Bao la penalti la Sadio Mane liliihakilkishia Liverpool ushindi wa kombe la kimataifa.

Salah na mshambuliaji wa Senegal Mane walikuwa wanacheza kwa mara ya kwanza tangu mataifa yao kuondolewa katika kombe la dunia katika awamu ya muondoano.

Bernado Silva wa Manchester City ambaye timu yake ya Ureno iliondolewa katika mechi ya kufuzu kwa robo fainali alicheza kwa mara ya kwanza, lakini City bado walikosa huduma za wachezaji 15 walioshiriki katika kombe la dunia Urusi.

''Ni kitu kizuri tulichofanya dhidi ya Liverpool waliotinga fainali ya kombe la vilabu bingwa katika dakika 75'', alisema kocha Pep Guardiola baada ya mechi hiyo.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mchezaji mpya wa Manchester City Riyad Mahrez (kushoto alicheza dhidi ya Liverpool

Lukas Nmecha alikaribia kuifungia City naye Curtis Jones angeishindia Liverpool penalti kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika.

Mchezo huo uliimarika baada ya Mane aliyekuwa akivalia jezi nambari 10 aliyopewa msimu huu mpya na Sane kuingizwa kama nguvu mpya.

Na City ilipovamia lango la Liverpool kwa kasi baada ya shambulio la Domonic Solanke kudaiwa kuotea , Sane aliwachenga mabeki wa Liverpool kabla ya kufunga katika kona ya goli.

Salah alisawazisha mambo na kujwa 1-1 muda mfupi baada ya kuingia katika nafasi ya Jones , akifunga kwa kichwa krosi iliopigwa na Rafa Camacho baada ya kuwachwa pekee.

Mane baadaye alifunga mkwaju wa penalti baada ya Solanke kuchezewa visivyo katika eneo hatari.

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mkufunzi wa Manchester City Pep Guardiola (kushoto) anaamkuana kwa mkono na mwenzake wa Liverpool Jurgen Klopp