Magufuli amteua Jokate Mwegelo kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe

Joketo Mwegelo Haki miliki ya picha Joketo Mwegelo/Instagram
Image caption Mlimbwende wa Tanzania Joketo Mwegelo atauliwa katika kuwa mkuu wa Wilaya katika mabadiliko yaliofanywa na rais John Pombe Magufuli

Rais wa Jahmhuri ya Tanzania John Pombe Magufuli alifanya mabadiliko katika nyadhfa za uongozi wa wizara na utawala wa miji.

Katika hafla iliotangazwa moja kwa moja kupitia runinga , Magufuli alimteua Profesa Joseph Buchweshaija kuwa katibu katika wizara ya viwanda, biashara na uwekezaji alkichukua mahala pake Profesa Elisate Ole-Gabriel ambaye amehamishwa hadi katika wizara ya mifugo na uvuvi.

Pia alimteua kamishna wa Kinondoni Bwana Ally Hapi kuwa Mkuu wa mkoa wa Iringa .

Rais pia alimchagua mlimbwende maarufu bi Jokate Mwegelo kuwa mkuu wa wilaya ya Kisarawe.

Katika tangazo hilo, rais Magufuli pia aliwateua baadhi ya wanasiasa wa upinzani waliojiunga na chama tawala CCM kuwa wakuu wa wilaya na makatibu tawala wa mikoa

Wanasiasa hao ni Moses Machali {Nanyumbu} na Petrobas Katambi {Dodoma}.

Kiongozi huyo pia alimteua mwandishi habari wa zamani wa shirika la habari la TBC bwana Jerry Muro kuwa mkuu mpya wa wilaya ya Arumeru .

Naye Kada wa zamani wa Chadema aliyejiunga na CCM bwana David Kafulila ameteuliwa kuwa katibu tawala wa Songwe.

Mkurugenzi wa mawasiliano ya Ikulu nchini Tanzania Gerson Msigwa alikuwa ametoa notisi kuhusu mabadiliko hayo.

Mada zinazohusiana

Maelezo zaidi kuhusu taarifa hii