United yaiangamiza Real Madrid, Barcelona hoi kwa Roma

Mfungaji wa goli la ushindi la United kiungo Ander Herrera

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Mfungaji wa goli la ushindi la United kiungo Ander Herrera

Michezo minne ya kimataifa ya kirafiki imemalizika asubuhi hii kwa Manchester United wakicheza mchezo wao wa mwisho wa maandalizi ya kujianda na msimu mpya wa ligi wamewachapa Real Madrid kwa magoli 2-1

Alexis Sanchez alianza kuipa United goli la kuongoza dakika ya 18 kisha kiungo Ander Herrera akaongeza goli la pili

Mfaransa Karim Benzema akawapa Madrid goli pekee la mchezo huo katika dakika ya 45 ya mchezo.

Goli pekee la Georges-Kévin N'Koudou likawapa Tottenham Hotspur ushindi wa goli 1-0 dhidi AC Milan.

As Roma wametakata kwa kuifunga Barcelona kwa magoli 4-2. magoli ya Barcelona yalifungwa na Rafinha na mchezaji mpya Malcon akifunga goli moja.

As Roma walipata magoli yao kupitia kwa Stephan El Shaarawy,Alessandro Florenzi,,Bryan Cristante,Diego Perotti