Tetesi za soka Ulaya Jumatano: Zidane, Modric, Lewandowski, Hazard, Willian, Mignolet

Zinedine Zidane

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

Zinedine Zidani anasakwa na Manchester United kuchukua nafasi ya Jose Mourinho

Manchester United wanamtaka kocha wa zamani wa Real Madrid Zinedine Zidane kuichukua nafasi ya Jose Mourinho kama meneja ikiwa Mourinho ataondoka klabu ya Old Trafford (Sun)

Inter Milan wanataka kusaini mkataba na mchezaji wa safu ya kati wa Real Madrid Mcroatia Luka Modric, mwenye umri wa miaka 32, ambaye yuko mapumzikoni kwa sasa nchini Italia. (Mail)

Chanzo cha picha, Getty Images

Maelezo ya picha,

The Blues wanatumai kwa kumtoa mchezaji wa safu ya kati N'Golo Kante kwa mkataba mpya wa £290,000

Chelsea inatumai kuipiku Real kwa kusaini mkataba na mchezaji wa wa safu ya mashambulizi wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski mwenye umri wa miaka 29. (Star)

The Blues wanatumai kwa kumtoa mchezaji wa safu ya kati N'Golo Kante kwa mkataba mpya wa £290,000- wa kila wiki ikiwa wanaweza pia kumshawishi mshambuliaji wa Ubelgiji Eden Hazard, mwenye umri wa miaka 27, kuendelea kubaki katika Stamford Bridge. (Evening Standard)

Hata hivyo Paris St-Germain hawakati tamaa ya kusaini mkataba na mchezaji wa kimataifa wa timu ya Ufaransa Kante alie na umri wa miaka 27. (mirror)

Maelezo ya picha,

Barcelona imeazimia kumchukua mlinda lango wa tiumu ya Ubelgiji Simon Mignolet

Chelsea bado hawajaridhishwa na kuchelewa kurejea kwa winga wa Brazil Willian kwenye klabu hiyo kwasabau ya masuala ya paspoti, huku mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 29 akiwa bado hajaripoti kwenye mazoezi ya kabla ya msimu . (Times - subscription required)

Mchezaji wa Liverpool mwenye umri wa miaka 30 - mlinda lango wa Ubelgiji Simon Mignolet analengwa kuchukuliwa na Barcelona. (Sky Sports)

Maelezo ya picha,

Meneja wa Chelsea Maurizio Sarri amemkaribisha mshambuliaji wa timu ya Ubelgiji Michy Batshuayi siku zijazo

Mchezaji wa safu ya ulinzi Luke Shaw, mwenye umri wa miaka 23, anafurahia kuuona mwaka wa mwisho wa mkataba wake katika Manchester United, licha ya klabu ya Ujerumani ya Wolfsburg kumtaka mchezaji huyo wa kimataifa wa England (Mail).

Mshambuliaji wa timu ya Ubelgiji Michy Batshuayi, mwenye umri wa miaka 24, ameambiwa na meneja wa Chelsea Maurizio Sarri kwamba nafasi ijayo katika Stamford Bridge, huku Crystal Palace na Valencia wakionyesha utashi wa kumchukua .(RMC, via Sun)

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain amekubali kuchukuliwa kwa mkopo na timu ya AC Milan

Everton wanataka kusaini mkataba na mchezaji wa kiungo cha kati wa Urusi Denis Cheryshev, mweye umri wa miaka 27, kutoka Villarreal. (Marca, via Talksport)

Crystal Palace inatumai kusaini mkataba na mshambuliaji wa Ujerumani Max Meyer, mwenye umri wa miaka 22, kutoka Schalke na Mbrazil anayecheza katika safu ya kati Josef de Souza mwenye umri wa miaka 29 kutoka klabu ya Fenerbahce. (Star)

Maelezo ya picha,

Real Madrid walizungumza na mchezaji wa safu ya mashambulizi Liverpool na Misri Mohamed Salah

Mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain amekubali kuchukuliwa kwa mkopo wa msimu mzima na timu ya daraja la kwanza katika ligi ya Serie A upande wa AC Milan, ambayo itakuwa na chaguo la kumnunua mchezaji wa Argentina mwenye umri wa miaka 31-year-kwa £32m mwishoni mwa msimu. (Guardian)

Real Madrid walizungumza na mchezaji wa safu ya mashambulizi Liverpool na Misri Mohamed Salah mwenye umri wa miaka 26 wakitaka achukue nafasi ya Cristiano Ronaldo baada ya Ronaldo mwenye umri wa miaka 33 mchezaji wa timu ya taifa ya ureno kwenda Juventus. (El Pais, via Star)

Maelezo ya picha,

Ni wazi kwamba sasa mchezaji wa safu ya kati ya Ufaransa Steven N'Zonzi ataendelea kusalia Sevilla, licha ya fununu za awali kwamba Arsenal wanataka kumchukua

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Ufaransa Thierry Henry amekubali kuwa meneja mpya wa Misri. (King Fut, via Talksport)

Rais wa Sevilla Jose Castro amekuwa wazi kwamba anamtarajia mchezaji wa safu ya kati ya Ufaransa Steven N'Zonzi kuendelea kusalia katika klabuhiyo. N'Zonzi mwenye umri wa miaka 29- alidhaniwa kuwa Arsenal wanataka kumchukua (Metro)

Mshambuliaji wa Uhispania Fernando Llorente, mwenye umri wa miaka 33, anasema kuwa anataka kubakia Tottenham, licha ya kuwa hucheza pale nahodha wa tumu ya England Harry Kane, mwenye umri wa miaka 25 anaposhindwa kucheza. (Evening Standard)

Maelezo ya picha,

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal na Ufaransa Thierry Henry amekubali kuwa meneja mpya wa Misri

Newcastle walimtoa meneja Rafael Benitez kwa timu ya Uhispania kwa michuano ya Kombe la Dunia baada ya kufukuzwa kwa Julen Lopetegui. (COPE, via Express)

Shirikisho la kandanda kuendelea kuwa na mkurugenzi wa masuala ya kiufundi Dan Ashworth, ambae anataka kazi hiyo hiyo katika klabu ya Ligi ya Primia Brighton (Mirror)

Sampdoria wako tayari kuthibitisha hatua yao ya kusaini mkataba na Ronaldo Vieira, 20, kutoka Leeds United baada ya kukubali mkataba wa miaka mitano na kikosi cha tuimu ya England cha vijana walio na umri wa chini ya 21 anayechezea safu ya kati (Yorkshire Evening Post)