Tour du Rwanda: Samuel Mugisha awika mbio za baiskeli

Samuel Mugisha
Maelezo ya picha,

Samuel Mugisha akiwa katika mashindano ya Tour du Rwanda

Mwendesha baiskeli wa Rwanda Samuel Mugisha ameingia katika mji wa Huye kusini mwa Rwanda akiwa ndiye wa kwanza.

Ametumia muda wa saa tatu,dakika 8 na sekunde 56 kutimka kwenye Barabara yenye urefu wa kilometa 120.

Amemuacha nyuma kwenye nafasi ya pili mwenzie Uwizeye Jean Claude naye kutoka Rwanda kati yao kukiwa na tofauti ya sekunde 21.Haile Michael Mulu wa Ethiopia ameshika nafasi ya tatu.

Mshindi wa mzunguko wa kwanza wa jana Lagab Azzedine leo ameshindwa kuhimili barabara yenye kona na milima japo ya leo siyo mirefu sana;amechukua nafasi ya 5 kwa ujumla kati yake na mshindi wa kwanza kukiwa na tofauti ya dakika 3.

Siku ya kesho ambayo itakuwa ya tatu washindani watatoka mjini Huye na kuelekea katika mji wa Musanze,kaskazini mwa Rwanda kilomita 200.Huu ndio mzunguko mkali zaidi katika mashindano haya na kiashiria cha mshindi wa mashindano haya ya mbio za baiskeli.