Wachezaji 9 ambao huenda wakahama klabu zao kabla ya siku ya mwisho Alhamisi

Muda unakwenda mbio: Tarehe ya mwisho ya wachezaji kuhama ni Alhamisi hii itashuhudia vilabu vikinga'ng'ana kufikia mikataba.

Je Tottenham hatimaye watamsaini mchezaji? Anthony Martial atabaki Manchester United?

BBC inaangazia wachezji watano ambao huenda wangafunganya virago kabla ya tarehe ya mwisho.

Toby Alderweireld (Tottenham)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Toby Alderweireld
Nafasi: Mlinzi Miaka: 29
2017-18 Mechi za Ligi ya Premier: 15 Amehusiswa na: Manchester United

Mlinzi huyu Mbelgiji Alderweireld alikuwa na wakati mgumu kudumisha nafasi yake huko Tottenham baada ya jeraha kumweka nje msimu uliopita.

Mkataba wa Alderweireld unaisha mwisho wa msimu na kutokana na kuwa Manchester United wanammezea mate bei aliyowekewa ya pauni milioni 75 itakuwa kizuizi.

Jack Grealish (Aston Villa)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Jack Grealish (Aston Villa)
Nafasi: Kiungo wa kati Umri: 22
2017-18 Mechi za Championship League: 30, mabao 3 Amehusishwa na: Tottenham, Chelsea

Mchezaji wa England wa kikosi cha wachezaji wa chini ya miaka 21 alifanya vizuri wakati Villa walikuwa waking'ang'ania ubingwa ambapo walishindwa na Fulham.

Aston Villa wana matatizo ya kifedha na Grealish amewavutia Tottenham ambao wanataka kumsaini kwa pauni milioni 20 lakini meneja Steve Bruce anahitaji mara mbili pesa hizo.

Danny Ings (Liverpool)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Danny Ings (Liverpool)
Nafasi: Mshambuliaji Umri: 26
2017-18 Mechi za Premier League: 8, magoli 1 Amehusishwa na: Crystal Palace, Southampton, Leicester, Newcastle

Mshambuliaji huyu wa England amepitia misimu mitatu smigumu huko Anfield na kafunga tu bao moja wakati wa mechi za Ligi ya Primia msimu uliopita.

Hilo hata hivyo halijawazuia the Reds kumwekea bei ya pauni milioni 20 mchezaji huyo huku ripoti zikisema kuwa Crystal Palace huenda wakamsaini.

Harry Maguire (Leicester)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Harry Maguire (Leicester)
Nafasi: Mlinzi Umri: 25
2017-18 Mechi za Premier League: 38, mabao 2 Amehusishwa na: Manchester United

Beki huyu amekuwa tegemeo kubwa kwa klabu yake na pia timu ya taifa.

Jose Mourinho anamwinda kwa mkataba wa pauani milioni 65 licha ya Leicester nao kutajwa kumwinda kwa pauni milioni 80 ambayo itakuwa ni rekodi ya dunia kwa mlinzi.

Anthony Martial (Manchester United)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Anthony Martial (Manchester United)
Nafasi: Wing'a Umri: 22
2017-18 Mechi za Premier League: 30 mabao 9 Amehusishwa na: Tottenham, Chelsea, Paris St-Germain

Martial amekuwa na wakati mgumu kuwa katika kikosi cha kwanza tangu Alexis Sanchez awasili na alikosa nafasi katika kikosi cha Ufaransa kilichoshinda kombe la dunia.

Mourinho hakufurahishwa baada Martial kuondoka kwenye safari ya Marekani ya mechi za maandalizi na kurudi Ufarana kuwepo wakati wake anajifungua mtoto wa pili na anatarajai kumuuza pauni milioni 80.

Simon Mignolet (Liverpool)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Simon Mignolet (Liverpool)
Nafasi: Mlinda Lango Umri: 30
2017-18 Mechi za Premier League: 10 Amehusishwa na: Barcelona, Besiktas

Kipa huyu mbelgiji alikuwa namba mbili kwa Karius lakini ameshuka zaidi baada ya kuwasili kwa raia wa Brazil Alisson kutoka Roma.

La kushangaza ni kuwa mabingwa wa La Liga Barcelona wanataka kumfanya Mignolet namba mbili baada ya Marc-Andre Ter Stegen, , huku Besiktas wakimmezea mate wanapomtafuta kipa mpya baada ya kumuuza Fabri kwenda Faulham

Aaron Ramsey (Arsenal)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Aaron Ramsey (Arsenal)
Nafasi: Safu ya kati Umri: 27
2017-18 Mechi za Premier League: 24, mabao 7 Amehusishwa na: Chelsea, Liverpool

Mchezaji huyu wa kimataifa wa Wales Ramsey amemaliza msimu 10 huko Arsenal akicheza zaidi ya mechi 300 lakini huenda akakumbwa na changamoto mpya kwenye mwaka misho mkataba wake.

Meneja mpya Unai Emery alimtajaa Ramsey kama mchezaji muhimu lakini mahasimu Chelsea wanaripotiwa kujipanga na pauni milioni 35 na hata Liverpool.

Willian (Chelsea)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Willian (Chelsea)
Nafasi: Wing'a Umri: 29
2017-18 Mechi za Premier League: 36, mabao 6 Amehusishwa na: Barcelona, Real Madrid, Manchester United

Wing'a mwenye bidii alicheza kwenye mechi zote za kombe la dunia za Brazil

Willian alikosa mazoezi ya msimu mpya kutokana na tatizo kwenye na pasipoti yake na anaweza kuelekea Real Madrid kwa pauni milioni 65.

Wilfried Zaha (Crystal Palace)

Haki miliki ya picha Getty Images
Image caption Wilfried Zaha (Crystal Palace)
Nafasi: Wing'a Umri: 25
2017-18 Mechi za Premier League : 29, mabao 9 Amehusishwa na: Borussia Dortmund, Chelsea, Tottenham

Licha ya kutocheza wiki tano za kwanza msimu uliopita Zaha aliwafungia palace bao 9.

Meneja Roy Hodgson anasema anataka raia huyo wa Ivory Coast kubaki lakini pesa nyingi zinaweza kuwaweka kwenye majaribio ya kumuuza.

Mada zinazohusiana